HABARI KUU
Wakili wa kujitegema nchini Wakili Peter Madeleka amesema wanajiandaa kufungua shauri la fidia ya shilingi za Kitanzania bilioni 36 dhidi ya mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar es salam Hassan Bomboko kwa udhalilishaji wa watu 36 alioagiza wamakatwe akiwatuhumu kujihusisha na biashara ya ngono na kisha kuachiliwa huru.
Wakili Madeleka ametoa kauli hiyo akizungumza na Watetezi tv na kuongeza kuwa hadi sasa watu hao ambao ni Wanawake na wanaume hawajasomewa mashtaka licha ya jana 19 June 2024 kupelekwa mahakamani .
Amesema tayari wameshajiandaa kwa ajili ya shauri hilo kwa lengo la kudai haki za watuhumiwa hao ambao amedai wanakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa Haki za Binadamu ikiwemo kunyimwa taulo za kike kwa wanawake ambao wapo katika siku zao.
Mkuu wa wilaya ya Ubungo jijini Dar es salam Hassan Bomboko mwishoni mwa wiki iliyopita aliendesha Oparesheni ya kukamata wanaojihusisha na Biashara ya ngono katika wilaya hiyo.