MICHEZO
Shirikisho la soka la Nigeria limekanusha kuhusu machapisho ya mtandaoni siku ya Jumatano kwamba Bodi inayosimamia Kandanda imempiga marufuku mshambuliaji wa Super Eagles, Victor Osimhen katika timu hiyo kutokana na kulikosoa shirikisho kwenye mitandao ya kijamii siku chache zilizopita.
Katibu mkuu wa NFF, Dkt. Mohammed Sanusi alieleza kushangazwa na taarifa hizo, akisema shirikisho hilo halijaagiza utaratibu wala mchakato wa kumfungia mchezaji huyo kuitumikia timu ya Taifa.
NFF inaviomba vyombo vya habari kuunga mkono chombo hicho ili kutatua masuala kwa njia chanya katika kukuza soka badala ya kufukua mzozo amabao hauna manufaa kwa mpira wa miguu.
Amesema lengo lao kwa sasa ni kusuluhisha masuala yote yanayohusu Super Eagles na kutazama mbele hasa katika kutafuta tiketi ya kufuzu kwa AFCON 2025 na mechi sita zilizosalia za kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA la 2026.