RAIS WA GUINEA BISSAU KUZURU TANZANIA KIKAZI

0:00

10 / 100

HABARI KUU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kumpokea Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, Mhe. Umaro Sissoco Embaló tarehe 22 Juni, 2024 Ikulu jijini Dar es Salaam ambaye atakuwa nchini kwa ziara ya kikazi.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais wa Guinea-Bissau kufanya ziara nchini Tanzania tangu nchi hiyo ipate uhuru. Ziara hiyo itatoa fursa kwa nchi zote mbili kuimarisha ushirikiano na uhusiano ambao umedumu kwa muda mrefu ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Amilcar Cabral wa Guinea-Bissau wakati wa kupigania uhuru.

Wakati wa ziara hiyo, Marais hao wawili wanatarajia kuongoza mazungumzo rasmi ya kiserikali kati ya Tanzania na Guinea-Bissau na kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ushirikiano (General Framework Agreement) ambao utaongeza mahusiano kati ya nchi hizi mbili.

Mbali ya mazungumzo na Rais Samia, Rais Embaló atatembelea Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) na Makao Makuu ya Sekretarieti ya Taasisi ya Viongozi wa Afrika ya Kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria (ALMA) yaliyopo hapa nchini, ambapo yeye ni Mwenyekiti wa ALMA.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Spurs sink Man City, Man United thump...
LONDON, - Tottenham Hotspur beat Manchester City 2-1 with goals...
Read more
Arteta frustrated by Arsenal's loss at Newcastle
NEWCASTLE, England, 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 - Arsenal boss Mikel Arteta was disheartened...
Read more
MAJAMBAZI WAUA MLINZI KKKT WAPORA MAMILIONI ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
Read more
KWA DOCUMENTARY HII NITAWASHANGAA WANAYANGA WASIPOVUNJA...
Makala Fupi
Watu wanakuja na kuondoka,maisha yanakuja na kupita,matukio nayo yanakuja...
Read more
President Ruto Vows to Fund Church Completion,...
President William Ruto has pledged to provide financial support to...
Read more

Leave a Reply