UHUSIANO WA TIBA ZA SOKWE NA BINADAMU JINSI ULIVYO

0:00

9 / 100

Imegundulika kwamba sokwe hula miti ambayo ina uwezo wa kutuliza maumivu na kuzuia bakteria wanapoumwa, wanasayansi wamegundua.

Watafiti wamegundua hilo wakati wanafanya kazi ya uchunguzi katika msitu mmoja nchini Uganda ambako utafiti wao ulilenga kuangalia sokwe waliojeruhiwa au kuugua ili kujua iwapo walikuwa wanajitibu kwa mimea au la.

Wakati mnyama aliyejeruhiwa alipotafuta kitu maalumu kutoka kwenye mimea ili kula, watafiti walikusanya sampuli za mmea huo na wakafanya vipimo. Mimea mingi iliyopimwa imeonekana kuwa na nguvu za kupambana na bakteria.

Wanasayansi, ambao wamechapisha matokeo yao katika jarida la PLOS One, wanafikiri sokwe wanaweza kumsaidia mwanadamu katika kutafuta dawa mpya zinazotokana na miti.

“Hatuwezi kupima kila kitu katika misitu hii kwa sifa zake za dawa, mtafiti mkuu Dkt. Elodie Freymann, kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, amesema. “Kwa hivyo kwa nini tusifanyie vipimo mimea ambayo tuna habari hii – mimea ambayo sokwe wanaitafuta (wanapoumwa au kujeruhiwa)?”

Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Dkt. Freymann ametumia miezi kadhaa kufuata na kutazama kwa makini jamii mbili za sokwe katika Hifadhi ya Msitu Mkuu wa Budongo.

Pamoja na kutafuta dalili za maumivu – mnyama akichechemea au kuushika mwili wake kwa njia isiyo ya kawaida – yeye na wenzake walikusanya sampuli za kinyesi na mkojo ili kuangalia ugonjwa na maambukizi.

Walizidisha umakinifu wao wakati sokwe aliyejeruhiwa au mgonjwa alipotafuta kitu ambacho kwa kawaida huwa hawali – kama vile magome ya mti au maganda yama matunda.

“Tulikuwa tunatafuta dalili hizi za kitabia kwamba mimea inaweza kuwa dawa,” Dk Freymann ameelezea.

Kwa jumla, watafiti walikusanya sampuli 17 kutoka kwa aina 13 tofauti za mimea na kuzipeleka kufanyiwa majaribio na Dk Fabien Schultz, katika Chuo Kikuu cha Neubrandenburg cha Sayansi nchini Ujerumani.

See also  During menstruation, there are no specific activities that women universally should avoid, but there are some common recommendations and considerations to help manage comfort and health:

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MESSI HANA MPINZANI HUKU ...
MICHEZO Mwandishi nguli wa habari za michezo, Fabrizio Romano amethibitisha...
Read more
MAGAZETI YA LEO JUMAPILI YA 24,2023 ...
Magazeti Karibu Mtanzania, asubuhi hii ya leo uone kilichojiri kwenye...
Read more
WAASI WA CONGO WAWEKEWA VIKWAZO NA UMOJA...
HABARI KUU Umoja wa Mataifa umeweka vikwazo vya usafiri, silaha...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA HIVI LEO 06/07/2024
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
BURNA BOY AWEKA REKODI MPYA STAVERN FESTIVAL...
MICHEZO Waandaaji wa tamasha la muziki la STAVERN FESTIVAL la...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply