HABARI KUU
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC) Hassan Bomboko ametakiwa kulipa kiasi cha Sh. Bil 36 kutokana na sakata la ukamataji wanawake 36, wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya ukahaba.
Suala hilo limechukua sura mpya, baada ya DC huyo kupewa notisi ya kuwalipa kiasi hicho wanawake hao.
Notisi hiyo ya wiki mbili imeanza jana Alhamisi, Juni 20, 2024 na inalenga kuwalipa watuhumiwa hao 36 wanaodai kudhalilishwa kwa kuwaita ‘Dada Poa’ na kuwaweka rumande kwa siku tano kinyume na sheria.
Notisi hiyo imeandikwa na wakili wao kutoka tasisi ya Stalwart, Peter Madeleka ambaye amethibitisha kwamba tayari wameshaiwasilisha kwa kiongozi huyo.
DC Bomboko alisema alikuwa hajapokea notisi hiyo inayoelezwa amepelekewa. ” Sijapokea hiyo notisi. Muulizeni vizuri.” Alipotafutwa tena jioni hakupatikana.
Hivi karibuni iliwakamata ‘makahaba’ hao Ubungo, River Side na Sinza, bado inavuta hisia za wengi mitandaoni wakieleza inaingilia faragha za watu na inakiuka haki za binadamu.