KWANINI MAANDAMANO YA KENYA YANAMG’OA IGP KOOME?

0:00

10 / 100

HABARI KUU

Viongozi wa muungano wa upinzani wa Azimio siku ya Ijumaa wametoa wito wa kujiuzulu mara moja Inspekta Jenerali wa Polisi wa Kenya Japhet Koome na Mkuu wa Polisi wa Nairobi Adamson Bungei kwa mauaji ya Rex Kanyike Masai.

Katika kikao na wanahabari, kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka amebainisha kuwa wawili hao walishindwa katika majukumu yao ya kuwalinda Wakenya waliokuwa wakiandamana kwa amani kupinga Muswada wa Fedha wa 2024.

Pia amemtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Mashtaka kuwafungulia mashtaka Koome, Bungei na afisa aliyehusika na mauaji ya Rex.

Mwanasiasa huyo wa Azimio amehoji ni kwa nini maafisa wa polisi walichukua hatua kali dhidi ya waandamanaji ambao hawakuwa na silaha na wasio na vurugu huku akiomba haki itendeke na akataka afisa aliyehusika afikishwe mahakamani.

“Hili ni tukio la kusikitisha na lenye athari mbaya. Muungano wetu umefadhaishwa sana na mauaji ya Rex. Tuna kumbukumbu nyingi sana za misiba hii, na mawazo na maombi yetu yako pamoja na familia yake, marafiki, na jamii ambayo imepata hasara kubwa kama hii” Ameeleza Musyoka.

Maoni yake yameungwa mkono na mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino aliyeonya afisa huyo aidha ajisalimishe au akabiliane na ghadhabu za Wakenya.

Kanda za CCTV zilizosambazwa mtandaoni zilionesha afisa wa polisi akiwafyatulia risasi waandamanaji katika eneo la CBD mjini Nairobi Alhamisi usiku. Kufuatia tukio hilo, habari zilizuka kuwa Rex alijeruhiwa vibaya.

Gilian Munyau, mamake Rex amesema maafisa hao wangeweza kumkimbiza mwanawe hospitali kabla hajamwaga damu lakini walichagua kutofanya hivyo badala yake walimwambia kumwambia ”wacha akufe”

See also  Nine-try England hammer Japan to end losing run in style

Akihutubia wanahabari nje ya chumba cha kuhifadhia maiti cha City mnamo Ijumaa, Gilian alielezea masikitiko yake akisimulia jinsi alivyopokea habari za kupigwa risasi kwa mwanawe mwendo wa saa saba usiku.

Imeelezwa kuwa Rex aliaga dunia kutokana na kutokwa na damu nyingi. Inaripotiwa kwamba alitumia zaidi ya dakika 20 kujaribu kutafuta matibabu kabla ya kukimbizwa katika Kituo cha Matibabu cha Bliss kando ya barabara ya Moi ambapo alithibitishwa kufariki alipofika.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Girona coach laments lack of depth after...
Girona have to cope with the absence of injured key...
Read more
7 BENEFITS OF EARLY MORNING SEX
❤ Having sex in the morning might just be the...
Read more
Mpango amwakilisha Rais Samia Kwenye Mazishi ya...
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amemwakilisha Rais Samia Suluhu...
Read more
SILENT SEX STRUGGLES MARRIED PEOPLE GO THROUGH
A SPOUSE WHO WANTS TOO MUCH SEX:- Some are married...
Read more
KASI ONGEZEKO "SINGLE MOTHERS" SASA YATISHA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Leave a Reply