Je Wafanyabiashara Tanzania wako Tayari kugoma?

0

0:00

HABARI KUU

Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania imekanusha taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii leo, Jumamosi Juni 22.2024 zikidai kuwa wafanyabishara nchini wameitisha mgomo kuanzia Jumatatu ya Juni 24.2024

Akizungumza na wanahabari usiku huu, jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Hamisi Livembe amesema kuwa jumuiya hiyo haijakaa kikao chochote kilichoazimia kuitisha kwa mgomo huo, badala yake wafanyabishara hao walikuwa na malalamiko ya baadhi ya hoja za kikodi siku za hivi karibuni hata hivyo viongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania wakiongozwa na yeye mwenyewe (Hamisi Livembe) walikwenda jijini Dodoma kwa ajili ya kujadiliana na serikali ambapo baada ya mazungumzo ya pande hizo mbili hatimaye muafaka umefikiwa, na kwamba maamuzi yaliyofikiwa yatatangazwa na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akihitimisha hoja ya bajeti kuu ya serikali Bungeni hivi karibuni

Amesema baada ya viongozi hao kupata taarifa za uwepo wa vipeperushi na matangazo yanayosambaa mitandaoni kuhusiana na jambo hilo wamechukua uamuzi wa kuwasiliana na viongozi wote wa jumuiya hiyo kutoka kwenye mikoa na wilaya mbalimbali nchini, ikiwemo uongozi wa soko la kimataifa la Kariakoo, Dar es Salaam lakini kote huko wamekana kuutambua mgomo huo

Livembe ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa jamii kupuuza taarifa hizo na kwamba uwepo wake hauna uhusiano wa moja kwa moja na wafanyabishara nchini, kama ilivyokuwa ikidhaniwa

Ameendelea kufafanua kuwa wafanyabishara wote nchini wanatambua njia na taratibu za kufuatilia mambo yao ikiwemo kufikisha kero na malalamiko yanayowakabili kwa viongozi wao

Taarifa iliyosambaa awali ilidai kuwa wafanyabishara nchini wameitisha mgomo unaoenda sambamba na kufunga maduka yao kuanzia Jumatatu Juni 24.2024 ambapo ilionesha kuwa wafanyabaishara hao wana madai takribani 14 wanayotaka kushughulikiwa na serikali miongoni mwake likiwemo suala la kushinikiza kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji madai ambayo yamekanushwa vikali na Livembe.

See also  Mambo 6 Muhimu ya kuzingatia kwenye kilimo cha Papai ili ufanikiwe.
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading