Kwanini Rais HUSSEIN MWINYI anapigiwa Chapuo Kuiongoza Zanzibar kwa Miaka Saba Badala ya Mitano?

0:00

9 / 100

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Said Dimwa, amesema Wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC – CCM Taifa Zanzibar, wamepitisha pendekezo la kuishauri Kamati Maalum ya NEC kuridhia kuongeza muda wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi kuongoza Nchi katika muhula wake wa kwanza kwa kipindi cha miaka saba badala ya mitano wakisema kwa kazi nzuri anayofanya Dkt. Mwinyi itakuwa ni hasara kufanya Uchaguzi mwaka 2025.

Dkt. Dimwa amesema hayo wakati akifunga Mkutano wa Baraza Kuu la UVCCM Wilaya Dimami kichama Zanzibar uliofanyika katika Ofisi za Wilaya hiyo Kiembesamaki.

Dkt.Dimwa amesema maamuzi hayo ya kumuongezea muda wa kuongoza Nchi Dk.Mwinyi yanatokana na kuridhishwa na kasi yake ya kiutendaji katika kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa zaidi ya asilimia 100 ndani ya kipindi miaka mitatu na miezi kadhaa toka aingie madarakani na kwamba Wazanzibar wanampenda, kumthamini na kuridhishwa na utendaji wa Dk.Mwinyi kwani amekuwa Kiongozi bora katika kutatua kero za Wananchi kupitia uimarisha wa Sekta mbalimbali za umma na binafsi.

Dkt.Dimwa amesema CCM Zanzibar imeona Serikali kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 ni hasara na matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi kwani wananchi wanahitaji maendeleo endelevu hivyo Rais Dk.Mwinyi anafaa kuongezewa muda ili Zanzibar iwe Nchi ya visiwa iliyoendelea kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

“Wajumbe wa Sektetarieti tumejadili na kutathimini kwa kina juu ya utendaji wa Rais Dk.Mwinyi, tukajiridhisha kuwa hakuna mbadala wake na anastahiki aongoze Nchi kwa kipindi cha miaka saba ili apate muda mzuri wa kufanya Mapinduzi ya kimaendeleo katika nyanja za kiuchumi na kijamii, maamuzi yetu yatafuata taratibu za kikatiba na kikanuni kwa kuyawasilisha katika vikao vya ngazi za juu ili vitoe baraka zake ili hoja hii ikapitishwe katika Baraza la Wawakilishi Zanzibar ili yaendelee kufanyika mabadiliko ya baadhi ya vipengele vya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kwa lengo kuhakikisha tunafanya Uchaguzi Mkuu wa dola kwa kila baada ya miaka saba”

See also  Undercover Detectives Intercept Suspected Drug Smuggler at JKIA

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

KEVIN DE BRUYNE AACHWA UBELGIJI
MICHEZO Kevin De Bruyne ameachwa nje ya kikosi cha Ubelgiji...
Read more
NBA roundup: Luka Doncic powers Mavs past...
Luka Doncic had 32 points, nine rebounds and seven assists...
Read more
CHADEMA YAONA KASORO MITAALA MIPYA YA ELIMU...
Magazeti Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao zake,
Read more
SUALA LA PACOME NA CAREN SIMBA LIKO...
NYOTA WETU Mrembo Caren Simba amejikuta kwenye wakati mgumu wa...
Read more
Djokovic said that he hired Murray as...
BUENOS AIRES, Argentina 🇦🇷 — Hiring Andy Murray as his...
Read more

Leave a Reply