KWANINI TANZANIA INAPANGA KUFUNGA SHUGHULI ZA UVUVI KWENYE ZIWA VICTORIA?

0:00

9 / 100

HABARI KUU

MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA UVUVI NA UKUZAJI VIUMBE MAJI LA EAC WAFANYIKA ARUSHA

Mkutano wa Kawaida wa Sita wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji katika Ziwa Victoria la Jumuiya ya Afrika Mashariki unaendelea jijini Arusha katika ngazi ya Wataalam ikiwa ni maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wa Sekta hiyo wanaotarajiwa kukutana tarehe 31 Mei 2024. 

 Mkutano huo wa siku tano terehe 27-31 Mei 2024, unalenga kufanya tathimini ya utekelezaji wa maagizo, maamuzi na makubaliano yaliyofikiwa kwenye musuala mbalimbali katika mikutano iliyopita ya Baraza hilo, ikiwemo masuala ya kiutawala, utekelezaji wa programu na miradi ya Jumuiya inayoratibiwa na kutekelezwa na Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ambayo inasimamiwa na Baraza hilo. 

 Tathimini na majadiliano yakayofanyika katika mkutano huo pamoja na masuala mengine ni mahsusi katika kukuza sekta ya uvuvi na ustawi wa viumbe maji ikiwemo kuendeleza ufugaji samaki endelevu katika Bonde la Ziwa Victoria na kuweka mikakati ya pamoja ya kuzuia na kupambana na magojwa yanayoathiri ustawi wa samaki na viumbe maji.

Mbali na hayo mkutano huo umepoke taarifa ya maandalizi ya mkutano wa kikanda wa wadau wa tasnia ya ukuzaji viumbemaji katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa Agosti, 2024 Jijini Mwanza. 

Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya EAC yenye Makao Makuu yake mjini Jinja, Uganda chini ya usimamizi wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uvuvi na Ukuzaji Viumbemaji inajukumu la kuratibu na kusimamia uendelezaji wa rasilimali za uvuvi na ukuzaji viumbe maji katika Jumuiya. 

See also  RWANDA YAIPINGA MAREKANI KUHUSU VITA YA CONGO

Miongoni mwa miradi inayotekelezwa na Taasisi hiyo ni pamoja uendeshaji wa boti katika ziwa Victoria zinazosaidia shughuli za doria na utafiti wa masuala mbalimbali ya samaki na viumbemaji na mradi wa UE-EAC TRUE-FISH unaolenga kukuza ufugaji samaki endelevu katika bonde hilo.

Mradi mwingine ni wa ECOFISH ambao umejikita katika kuendeleza matumizi bora na usimamizi endelevu wa rasilimali samaki na viumbemaji kwa kuweka sera na mifumo inayohimiza ufanisi ikiwemo matumizi ya mbinu bora za uvuvi.

Mkutano huo Ngazi ya Wataalam umehudhuriwa na nchi ya Tanzania, Kenya, Burundi na Uganda

Kutokana na makubaliano yaliyofanyika kati ya Wanachama wa Jumuiya ya Afrika, mkakati wa kulinda Ziwa victoria na viumbe wake ndio sababu inayotajwa Tanzania kufanya uamuzi wa kusitisha shughuli za uvuvi ndani ya ziwa hilo.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Adam Peaty lost a race but shed...
The 29-year-old Briton, whose battle with drink and mental health...
Read more
WHY LOVE IS THE SIMPLE THINGS
Love is making the bed together when you wake up...
Read more
How a girl supposed to attract man...
LOVE TIPS ❤ 1- change your character for good .2-...
Read more
Indiana Fever guard Caitlin Clark continued her...
The 22-year-old led the Fever to an 84-80 win against...
Read more
Kwanini Tanzania inailipa Kampuni ya Indiana Dola...
Serikali ya Tanzania imekubali kuilipa kampuni ya Australia, Indiana Resources...
Read more

Leave a Reply