Rais HUSSEIN MWINYI Awapiga Chenga “Machawa” Zanzibar

0:00

9 / 100

Serikali ya Zanzibar imesema Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi ni Muumini wa kufuata Katiba na Sheria za Nchi na kusisitiza kwamba maoni yanayopendekaza aongezewe muda wa kubakia madarakani kwa miaka saba badala ya miaka mitano iliyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar sio ya Rais Mwinyi wala sio ya CCM Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu ya Zanzibar, Charles Hilary leo June 24,2024 imesema “Hivi karibuni kumetolewa maoni yanayopendekaza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi aongezewe muda wa kubakia madarakani kwa miaka saba badala ya miaka mitano iliyoainishwa katika Katiba ya Zanzibar”

“Maoni hayo yamekwenda mbali zaidi hata kutaka Uchaguzi Mkuu wa mwakani kumchagua Rais wa Zanzibar usifanyike, jambo hili halina tija wala faida kwa Nchi yetu na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chenye kufuata misingi ya demokrasia”

Rais Dk. Mwinyi ataendelea kuheshimu utaratibu uliowekwa wa Rais kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano na amewasihi wale wote wenye mawazo tofauti na hayo wafunge mjadala huo”


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Aziz Ki hajasaini na sababu ni hizi zipo kwenye hela ya usajili na mshahara
Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading