Hali ilivyo katika mitaa mbalimbali ya soko kuu la Kariakoo lilipo Jiji Dar es Salaam, asubuhi ya leo Juni 24 2024, wafanyabiashara wamegoma kufungua maduka wakishinikiza serikali kutekeleza makubaliano yao waliyokubaliana mwaka jana 2023 katika kikao chao na waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Baadhi ya wafanyabiashara wamesema sababu kubwa iliyopelekea wao kufanya mgomo huu katika Soko la Kariakoo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kurudisha Kikosi Kazi (enforcement) kubwa zaidi kuliko ya awali iliyozuiliwa na Waziri Mkuu katika mkutano wa mwisho baina ya serikali na wafanyabiashara uliofanyika Mei 2023 katika viwanja vya mnazi mmoja.

Related Content
Related Content
Related News 
Mwanaharakati maarufu, Mange Kimambi, ameibua mjadala kuhusu uchaguzi wa ndani...
Ousmane Dembele has made positive strides in his second season...
Aden Duale, the nominated Environment Cabinet Secretary of Kenya, has...