Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Petro Magoti amepiga marufuku watu kuandaa shughuli za ngoma kama vile mdundiko, unyago na sherehe za muziki na kuruhusu wanafunzi kujumuika.
Amemuagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kisarawe endapo vitendo hivyo vitabainika akamate kuanzia mpiga ngoma, wazazi wa mtoto, aliyepewa tenda ya muziki hadi gari lililobeba muziki huo.
“Mh. OCD kwa wale viongozi wako wa kata ngoma ikikutwa anachezwa mwanafunzi, kamata anayepiga ngoma, kamata mama, kamata aliyepeleka muziki, gari lililopeleka muziki peleka kituoni, kama mtu anapewa tenda ya kuchezesha ngoma kwa wanafunzi waambie wasiende, tutakamata gari, tunafika polisi pale usiku tunatoboa matairi upepo hamna muziki utaletwa hapa halmashauri,”. amesema DC Magoti
Akizungumza
wakati akikabidhiwa ofisi na mtangulizi wake Fatma Nyangasa, Magoti amewataka pia walimu wanaoanzisha mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi wao waniandae, kwani akiwabaini atawashughulikia.
“Nimesikia kuna walimu wanapenda wanafunzi, sitaki kuwahukumu sijafika, naendelea kupokea data zangu. Kama wewe unatafuna watoto wetu ambao Mh. Rais analeta pesa yule Mtoto anakula anavaa anapendeza, yaani Mh. Rais anatoa matumizi wewe unakula!, serious?. amehoji Mkuu huyo wa Wilaya ya Kisarawe