Waandamaji zaidi ya Watano wameuwawa kwa risasi wakati Polisi wakipambana na Waandamanaji wanaopinga Muswada wa Fedha 2024
Chama cha Madaktari cha Kenya kimeripoti kusambaa kwa miili kadhaa ya Watu nje ya eneo la Bunge ambapo waandamanaji walivamia jengo hilo Jijini Nairobi
Wakati huohuo, Hospitali ya Taifa ya Kenyatta imeendelea kupokea idadi kubwa ya majeruhi asilimia kubwa wakiwa ni vijana
Kama Gen Z walivyoahidi kulizingira bunge na kuizima Kenya nzima kwa maandamano, ikiwa ni pamoja na kwenda Bungeni wamefanya hivyo, ambapo mpaka sasa wandamanaji wawili wanaripotiwa kupoteza maisha baada ya kupigwa risasi na polisi wanaotuliza ghasia.
Inasemeka zaidi ya wabunge 150 wamekwama bungeni baada ya waandamanaji kuvamia bungeni hapo. Baadhi waliweza kuchomoka kwa miguu huku wengine chini ya uangalizi mkali wa polisi.