JESHI LA KENYA KUPITA MTAANI KUTULIZA VURUGU

0:00

10 / 100

Rais wa Kenya William Ruto, ametangaza kuwa Jeshi la nchi hiyo na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, vitaingia mitaani ili kuhakikisha wanalinda usalama wa Watu na mali zao dhidi ya Waandamanaji wanaofanya kile alichokiita kwamba ni uhalifu.

Rais Ruto ameyasemayo wakati akihutubia Taifa nchi hiyo leo June 25,2024, kufuatia kukithiri kwa vurugu za maandamano ya wananchi waliokuwa wakipinga muswada unaojadiliwa Bungeni kuwa ni kandamizi kwao

Ruto amese “Miundombinu na vyombo vyote vilivyoanzishwa kwa ajili ya kuulinda Umma na Serikali vitasambazwa kulinda usalama wa nchi na kuirejesha nchi kwenye hali ya amani”

“Haikubaliki kuona wahalifu ambao wanajifanya Waandamanaji wa amani wanafanya ghasia dhidi ya Watu, Wabunge walioteuliwa na kuinajisi Katiba na kutegemea waachwe huru

“Tunapaswa kuutenga na kutofautisha uhalifu na demokrasia na uhuru wa kutoa maoni. Nitaendelea kuongoza Serikali ambayo itahakikisha inalinda usalama wa Raia wote na mali zao”

Amesema Rais Ruto wakati wa hotuba yake kwa nchi hiyo.

Wakati huo huo

Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyetta ametoa wito wa kupatikana kwa utulivu na amani kurejeshwa kufuatia maandamano makubwa Nchini humo na kuwataka Viongozi kutambua kuwa madaraka na mamlaka waliyonayo wamepewa na Wananchi hivyo kuwasikiliza Watu ni lazima na sio jambo la hiari.

Kenyatta ameutaka pia Uongozi kuchukua uamuzi sahihi wa kusikiliza na kutowapuuza Watu akisema vurugu kwa pande zote mbili sio suluhisho la matatizo “Wapendwa Wakenya nasimama nanyi na naomba Uongozi uzungumze na Wananchi, naomba amani na maelewano kwa kila Mkenya na sote tukumbuke Kenya ni kubwa zaidi kuliko mmoja wetu”

See also  WATU 9 WAFARIKI BAADA YA GARI LAO KUSOMBWA NA MAJI

“kama Rais wenu wa zamani nimeona uzito na ugumu wa kuiongoza Kenya, kwahiyo ninaomba hekima na ustaarabu uimarishwe na amani na maendeleo iwe kwetu sote Watoto wa Kenya” Mstaafu Uhuru Kenyatta.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

President Tinubu has approved the transition from...
Bola Tinubu, the ex-governor of Lagos State and the current...
Read more
MAUMIVU YA NAULI MPYA KUANZA HIVI LEO...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Cristiano Ronaldo etched his name in the...
In a groundbreaking achievement, football legend Cristiano Ronaldo has etched...
Read more
What signs does a man show when...
When a man loses interest in a relationship, his behavior...
Read more

Leave a Reply