Baada ya Taarifa za Leo Kupitia Kwa
Mwenyekiti wa Coastal Union, Bwana Steven Mguto kwamba wamerejesha Milioni 205 za Simba Sports.
Maswali Mengi ya Wadau yamekuwa yakihoji ni kwanini Coastal Union wanajiamini Kiasi hiki?
Kuna sehemu Wana hoja?
Okay twende tuone.
Simba Sports wao wanakubali kwamba ni kweli Pesa wamelipa nje ya muda ambao walikubaliana na Coastal Union Yani tarehe 10/6/2024 Badala ya 30/5/2024.
Lakini kwanza walitakiwa Kupata Barua ya rai kutoka Coastal Union kuwa tarehe ya mwisho ikivuka Mkataba unavunjika, hii hawakupata.
Barua ambayo Simba wanasema waliipata
kutoka kwa Coastal Union ni ya taarifa ya
kuvunjika Kwa Mkataba ambayo iliandikwa
tarehe 14/5/2024, yani siku 16 nyuma ya
Deadline.
Swali hapo linabaki Coastal Union walijuaje
Kwamba Simba Sports watavusha Deadline ya Malipo siku 16 nyuma?
Nitarudi hapa Baadae.
Barua nyingine ambayo Simba wanasema
waliipata ni ya kutoa Maelekezo ya Malipo ya Lameck Lawi ya tarehe 3/6/2024.
Swali hapa linakuwa huyu mchezaji anayombewa Malipo hapa si Mkataba wake ulivunjika Rasmi Tarehe 30/5/2024??
Turejee kwenye swali la pale juu kwamba
Coastal Union walijuaje Kwamba Simba
Sports hawataweza Kulipa Pesa Kwa Muda
uliopangwa siku 16 nyuma Kabla ya Tarehe ya Mwisho?
Hapa Coastal Union wanasema kulikuwa na
Makosa, hiyo Barua ya kuvunjika rasmi Kwa
Mkataba ilitakiwa Kusoma tarehe 14/6/2024 badala ya 14/5/2024.
Wanasema “It was Just
Sleeping of the Pen” ambayo kimahakama
inaeleweka.
Kuhusu Barua ya kutoa rai baada ya Deadline ya Malipo, Coastal Union wao wanasema hii inafanyika tu ikiwa wao wameshamhamisha Lameck Lawi kutoka kwenye Mfumo kwenda Simba Sports.
Na Vipi kuhusu mchezaji Pesa alichukua?
Yes Lameck Lawi amechukua Mil 130M.
Je, na yeye ameshairejesha kama Coastal Union walivyofanya?
Hakuna anayefahamu.
Coastal Union kurejesha Wana idhini ya
Lameck Lawi?
Kwasababu wanaweza
kurejesha Pesa wao lakini mchezaji anataka kucheza Simba Sports.
Upi Utakuwa Mwisho wa hili sakata? Lameck Lawi msimu ujao atacheza Coastal Union au Simba Sports?
Lakini watu wanahoji hii jeuri ya Coastal
Union Kuvimbiana na Simba inatokana na
taratibu peke yake au kuna nini kilichojificha?