Kulingana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), inaonesha kisukari na shinikizo la damu (presha ya juu) ni moja ya magonjwa yanayoweza kusababisha kupoteza uwezo wa kuona ( upofu).
Namna Kisukari kinavyosababisha Upotezaji wa Uwezo wa Kuona
🔴 Kisukari na Ugonjwa wa Retina.
Viwango vya juu vya sukari kwenye damu vinaweza kuharibu mishipa ya damu kwenye retina, tishu inayopokea mwanga nyuma ya jicho. hali ambayo kusababisha mishipa ya damu kutokwa na majimaji au kuvuja damu, ambayo inaweza kufanya uono kufifia na hatimaye kusababisha upofu kama ikiachwa bila matibabu.
🔴Kisukari na mtoto wa jicho
Mtoto wa jicho ni wingu linalofunika lensi wazi kawaida kwenye jicho lako. Lensi za kila mtu huanza kupata mawingu kadri wanavyozeeka. Lakini watu wenye kisukari wana uwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa jicho na kwa umri mdogo zaidi hali ambayo hupelekea uoni kupungua.
🔴Kisukari na shinikizo la damu ni vihatarishi vya
Presha ya macho.
Presha ya macho ni kundi la magonjwa ya macho yanayoharibu mishipa ya fahamu ya macho, kawaida kutokana na shinikizo kubwa la macho. Watu wenye kisukari, wana mara mbili zaidi ya kukuza presha ya macho, ambaye hupelekea kupoteza uoni moja kwa moja kwa mgonjwa.
Namna shinikizo la Damu linavyosababisha Upotezaji wa Uwezo wa Kuona;
🔴shinikizo la damu na ugonjwa wa retina-
Shinikizo la juu la damu lisilodhibitiwa linaweza kuharibu mishipa ya damu mwili mzima, ikiwa ni pamoja na ile ya kwenye jicho hali ambayo huweza kupelekea upofu moja kwa moja.
🔴Uharibifu wa mishipa ya fahamu ya macho:
Shinikizo la juu la damu pia linaweza kuharibu mishipa ya fahamu iliyo kwenye jicho, inayobeba ishara kutoka jicho hadi ubongo. Hii inaweza kusababisha upotezaji wa uwezo wa kuona, maumivu, na upofu.
Nini kinapaswa kufanywa?
🌟Kugundua mapema na kutibu kisukari na shinikizo la damu ni muhimu kuzuia kupoteza uwezo wa kuona.
🟣Uchunguzi wa mara kwa mara wa macho ni muhimu kwa watu wenye hali hizo.
🟣Dhibiti kiwango vya sukari kwenye damu ikiwa una kisukari.
🟣Dumisha uzito wenye afya.
🟣Fuata mlo ulioshauriwa na daktari.
🟣Fanya mazoezi mara kwa mara.
🟣Usivute sigara.
🟣Tembelea daktari wako kwa uchunguzi zaidi.