🌟 Ukweli ni kwamba, Kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha kumekuwa na ongezeko la ugonjwa wa kisukari kati ya watoto ambao awali ulikuwa ukionekana kwa watu wazima, Shirika la Afya Duniani limeonyesha kuongezeka kwa ugonjwa wa kisukari kwa miongo miwili iliyopita na hii inatukumbusha kuchukua tahadhari hususani kwa wazazi kuwa waangalifu na kuchukua hatua sahihi za kuzuia watoto wao wasipate ugonjwa wa kisukari na kuhakikisha afya zao ziko salama.
✨Zifuatazo ni aina za kisukari kwa watoto pamoja na visababishi vyake.
🔴Kisukari Aina ya Kwanza:Huu ni ugonjwa wa kinga ambapo mfumo wa kinga ya mwili unashambulia seli zinazozalisha insulini kwenye kongosho. Hii husababisha upungufu wa insulini, homoni inayohitajika kudhibiti kiwango cha sukari mwilini. Aina ya Kwanza ni aina ya kisukari ya kawaida kwa watoto.
🔴Kisukari Aina ya Pili: Hii ni nadra kwa watoto kuliko na huwapata sana watu wazima. Kwenye kisukari aina ya pili, mwili hauzalishi insulini ya kutosha au unakuwa na upinzani wa athari zake na kupeleka mtu kupata kisukari.
Visababishi na Mambo ya Hatari:
Kisukari Aina ya Kwanza.
🔴Visababishi:
Sababu kamili haijulikani, lakini inaaminiwa kwamba husababishwa na hitilafu za vinasaba (urithi) na mabadiliko ya mazingira.
🟣 Vihatarishi
🍀 Historia ya kisukari kwenye familia.
🍀 Magonjwa ya kinga za mwili zinazoshabulia mwili.
Kisukari Aina ya Pili:
🟣Vihatarishi
🍀Historia ya kisukari kwenye familia
🍀Unene kupita kiasi au kiribatumbo
🍀 Kutokuwa na mazoezi ya kimwili
🍀 Kuzaliwa na mama aliye na kisukari cha mimba
Kinga: Hakuna njia ya uhakika ya kuzuia kisukari aina ya kwanza, Ila kwa Kisukari aina ya pili kinaweza kuzuiwa kwa njia zifuatazo;
🟣 Kuwa na uzito unaofaa
🟣 Kuwapa watoto mlo kamili
🟣 Kufanya mazoezi mara kwa mara
🟣 Kupunguza vyakula vya kusindikwa vyenye sukari nyingi( Junk foods).