Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Judith Suminwa Tuluka amesema kwamba Serikali ya Kinshasa haitaki mazungumzo na Rwanda kwa sababu inaituhumu kuwasaidia Waasi wa Kundi la M 23 huko Mashariki ya nchi yake.
Alipoitembelea kambi ya wakimbizi karibu na Goma AlhamisI, Tuluka ametoa wito kwa washirika wakuu wa Congo kuchukua hatua kali na vikwazo dhidi ya Kigali.
Alhamisi hiyo Rais wa Angola Joao Lourenco akiwa katika ziara huko Ivory Coast amesema kwamba mazungumzo yanaendelea katika kiwango cha mawaziri kwa lengo la kuwaleta pamoja viongozi wa Rwanda na DRC kwa haraka iwezekanavyo ili kukubaliana juu ya kupatikana amani ya kudumu Mashariki ya Congo.
Angola imekuwa ikijaribu kupatanisha nchi hizo mbili kutokana na ugomvi katika Jimbo la Kivu ya Kaskazini ambako waasi wa M 23 wanadaiwa kuungwa mkono na Rwanda wamekuwa wakipigana na Jeshi la Serikali tangu mwishoni mwa 2021.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.