0:00
Mfanyabiashara ambaye pia aliwahi kuwa Mfadhili na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amefariki Dunia wakati akiendelea na matibabu Nchini Marekani
Taarifa iliyotolewa imeeleza kwa mujibu wa mtoto wa Manji, Mehbub Manji ni kuwa msiba huo umetokea Jumamosi Juni 29, 2024 katika Jimbo la Florida
Manji alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Quality Group Limited (QGL), pia, aliwahi kujihusisha na siasa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na kufanikiwa kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu.
Yusuf Manji mzaliwa wa tarehe 6/12/1974 (49).Mwaka 1995 alipokea na kuziendeleza rasmi biashara za Baba yake akiwa kijana wa miaka 20 tu.
Pia Yusuf Manji ameshawahi kuwa mdhamini wa Yanga kwa miaka ya nyuma kabla ya kuachia nafasi hiyo ya udhamini.
Related Posts 📫
Klabu ya Yanga itaweka kambi yake ya maandalizi nchini Urusi...
VIGO, Spain, 🇪🇸 - Celta Vigo fought back with two...
SIASA
Tume Huru ya uchaguzi nchini Rwanda imewaidhinisha watu watatu katika...
Novak Djokovic expects nothing less than a titanic duel with...
1.. Words are like keys; if you choose them right,...