Ugonjwa wa Saratani ya Tezi Dume

0:00

12 / 100

MAANA YA TEZI DUME:

Tezi dume ni moja ya tezi la uzazi la kiume ambalo kila mwanaume analo. Tezi dume sio ugonjwa bali ni kiungo kama viungo vingine mwilini.

TEZI DUME INAPATIKANA WAPI KATIKA MWILI?

Tezi dume inapatikana chini ya kibofu cha mkojo na inazunguka njia ya mkojo toka kwenye kibofu kwenda kwenye uume.

KAZI ZA TEZI DUME KATIKA MFUMO WA UZAZI:

Kutengeneza majimaji ya uzazi wa mwanaume (shahawa) ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizotengenezwa kutoka kwenye korodani, ambapo wakati wa tendo la ndoa, mwanaume anapofika kileleni, tezi dume hukamulia majimaji (shahawa) ndani ya mrija wa mkojo na kutolewa pamoja na mbegu za kiume kama manii (Semen). Pia husaidia mbegu za kiume kubaki na uhai kwa muda unaostahili.

AINA ZA MAGONJWA YA TEZI DUME:

Kuna aina tatu za magonjwa ya tezi dume ambazo ni;
1) Maambukizi ya bakteria (Prostatitis).
2) Kukua kwa tezi dume ambalo sio saratani (Benign Prostate Hyperplasia-BPH)).
3) Saratani ya tezi dume.

Chanzo Cha Kupata Saratani Ya Tezi Dume:

Chanzo hasa cha saratani ya tezi dume hakijulikani, saratani hii ina uhusiano mkubwa na;

a) UMRI (Age).
Wanaume wenye umri kuanzia miaka 60 na kuendelea wapo katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.

b) KURITHI (Genetics).
Familia yenye historia na saratani hii ipo katika hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.

c) LISHE HATARISHI.
Ulaji kwa wingi wa nyama nyekundu, mafuta (samli), maziwa ya krimu hongeza hatari kubwa ya kupata saratani ya tezi dume.

d) UNENE ULIOKITHIRI (Obesity).

e) UKOSEFU WA MAZOEZI.

f) UPUNGUFU WA VIRUTUBISHO, mfano vitamini D.

g) MAAMBUKIZI YA MARA KWA MARA KWENYE TEZI DUME.

h) MATUMIZI YA POMBE KALI, NA UVUTAJI WA SIGARA.

i) UWEPO WA SUMU NYINGI MWILINI.

See also  Etinosa Idemudia defends Phyna against critics after she mistakenly called out soft drink brand

DALILI ZA SARATANI YA TEZI DUME:

Katika hatua za awali, dalili hazitofautiani sana na zile za kuvimba kwa tezi dume lisilokuwa saratani (Benign Prostate Hyperplasia).

Dalili hizo ni pamoja na;
a) Kusikia kupata haja ndogo mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

b) Haja ndogo kuchelewa kutoka unapoanza kukojoa.

c) Kutoa mkojo wenye mtiririko dhaifu na kuchuruzika kidogo kidogo baada ya kumaliza kukojoa.

d) Kujikakamua wakati wa kukojoa na kushindwa kumaliza mkojo wote.

e) Kutoa mkojo au manii yaliyochanganyika na damu.

f) Maumivu makali sehemu mbalimbali za mwili kama saratani imesambaa.

g) Kupungua uzito, kuhisi kichefuchefu, uchovu na kizunguzungu.

Kumbuka: Mtu mwenye tatizo katika tezi dume huanza kwa dalili ndogo ndogo sana mpaka mtu apate saratani ya tezi dume(prosate cancer) ujue amekaa na tatizo hilo kwa muda mrefu si chini ya miaka isiyopungua 10.

Hii hutokana na mrundikano wa mkojo unaobaki kwenye kibofu na kwenye mrija wa mkojo(urethra) wakati unakojoa ukiendelea kujirundika kwenye kibofu na mrija baada ya muda unazalisha”Uric acid” na ndio inatengeneza saratani (cancer).

Mara nyingi saratani ziko katika stage nne ambapo stage ya 1 na ya 2 ukiwahi unaweza kupona lakini ikishafika stage ya 3 na ya 4, hazitibiki bali unasaidiwa kupunguza makali kwa mionzi ukijitayarisha kupoteza maisha muda wowote.MATIBABU YA SARATANI YA TEZI DUME:

Watu wengi hukimbilia hospitali pindi wanapopatwa na madhara ya tezi dume na kujikuta wakipewa tiba ambazo huficha tatizo hilo kwa muda mfupi kisha tatizo hujirudia kwa kasi kubwa.
Tezi dume iliyotanuka haiwezi kutibika kwa njia za madawa yenye makemikali au Mitishamba, lakini madawa au upasuaji hupunguza maumivu ya dalili na kuzifanya zisizidi sana.
Kuna njia tatu za kudhibiti tezi dume iliyotanuka ambazo ni;

1) KUSUBIRI NA KUFUATILIA KWA UKARIBU NA DAKTARI

Imashauriwa kwamba kwa tatizo hili ni bora kuendelea kulichunguza bila kukimbilia tiba kali kama dawa, upasuaji na tiba kemikali, mpaka pale mtu atakapoona hakuna njia mbadala.

2) MADAWA.

Baadhi ya madawa wanayopewa wagonjwa wa saratani ya tezi dume yaligunduliwa miaka30 iliyopita yanasababisha athari kwenye ini, moyo, na kuvimbisha magoti,yamepigwa marufuku katika nchi haswa za ulaya.

3) UPASUAJI

Njia hii ambayo madaktari hutumia inapelekea ”70% ya wagonjwa kuwa mahanithi baada ya upasuaji, na 40% wanashindwa kuzuia mkojo kutoka wanapo banwa na haja ndogo.”

Kumbuka: Matibabu ya saratani ya tezi dume yanategemea hatua ya ugonjwa na umri wa mgonjwa.MADHARA YA UPASUAJI WA TEZI DUME:

Baada ya mgonjwa wa saratani ya tezi dume kufanyiwa upasuaji, madhara yafuatayo yanaweza kutokea;

1) Kukosa Uwezo wa Kufikia Mshindo Yani Hutoi Shahawa

 Wazee wengi hulalamika sana baada ya upasuaji wa tezi dume hivyo ushauri nasaha lazima utolewe ili mgonjwa ajue nini madhara yake kabla ya operation.

2) Kuziba Kwa Njia Ya Mkojo Kutokana Na Kuumia Kwa Njia Hiyo Wakati Wa Kufanyiwa Upasuaji

Baada ya upasuaji wa tezi dume, mgonjwa anapoendelea kupona kovu linaweza kuziba njia ya mkojo.

3) Shida Ya Kushindwa Kudhibiti Mkojo Usitoke Ovyo

Ni kawaida kwa mgonjwa kushindwa kudhibiti kutoka kwa mkojo katika siku za mwanzo baada ya operesheni. Hata hivyo hali hii hujirekebisha baada ya siku kadhaa kupita.

4) Kutokwa Na Damu Katika Siku Za Awali Baada Ya Upasuaji

Mara baada ya upasuaji wa tezi dume kupitia njia ya mkojo, Kidonda kwenye tezi dume kinaweza kuvuja damu ambayo itaonekana katika mkojo.

5) Ugumba

Kwa kawaida wakati wa tendo la ngono, mbegu za kiume kutoka kwenye korodani huingia kwenye urethra karibu na kijitundu cha kibofu cha mkojo. Wakati wa tendo la ndoa, misuli maalumu hufunga kijitundu hicho ili kuzuia mbegu zisiingie kwenye kibofu badala yake zielekee kwenye urethra ya katika uume. Hata hivyo, upasuaji wa tezi dume huondoa misuli hiyo na kufanya mbegu kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kuendelea kwenye urethra ya uume. Shahawa hizo hatimaye hutolewa nje ya kibofu pamoja na mkojo.Kinga Ya Saratani Ya Tezi Dume:

1) Fanya mazoezi ya mwili na uwe na uzito unaostahili ukilinganisha na urefu wako.
2) Kula vyakula vyenye mafuta kiasi na hasa ya mimea, vyakula vyenye asili/vyenye soya, vyakula vyenye” lycopene”(inapatikana kwenye nyanya), tikiti maji na matunda mengine, mboga za majani kwa wingi na samaki.

SULUHISHO LA KUDUMU LA SARATANI YA TEZI DUME

Tezi dume inatanuka kwa sababu ya upungufu wa madini na virutubisho ambavyo mwili Unavihitaji. Hivyo basi tumekuandalia progam maalumu kwa wenye changamoto hii ya kutanuka kwa tezi dume na mfumo wa uzazi wa mwanaume.

Tumewaandalia program ya lishe kamili na virutubisho muhimu. Bidhaa hizi ni vyakula, siyo dawa wala mitishamba. Zimetengenezwa kutoka kwenye vyakula ambavyo tungefaa kula kila siku na vina lishe kamili na virutubisho muhimu katika mwili wa mwanaume ili kutengeneza afya bora na Nadhifu.

See also  Mkuu wa Wilaya Morogoro Rebeca Nsemwa ameagiza kuchukuliwa hatua za kinidhamu Diwani Kata Mwembesongo Mhe.Ally Rashidi Kalungwana Kwa kitendo cha Kutumia vibaya madaraka yake kujenga vibanda vya biashara katika eneo la wazi Soko Kuu la chifu Kingalu Manispaa ya Morogoro

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Euro 2024 was not just a historic...
Four stalwarts - Ilkay Gundogan, Thomas Muller, Manuel Neuer and...
Read more
SAMIA ATOA NENO KUJIUZULU DANIEL CHONGOLO
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye Jamhuri yetu tukufu...
Read more
POLISI WAPEWA KIBALI KUMSHTAKI IGP
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
HOW TO APPROACH A WOMAN
Have confidence; not pride. Confidence is attractive, women detest pride. Women...
Read more
Pep Guardiola has made it clear he...
The striker has starred for City since arriving in the...
Read more

Leave a Reply