HARUFU MBAYA UKENI:
Kutokwa na harufu mbaya ukeni ni tatizo linalowasumbua wanawake wengi duniani, hususani wakati wa tendo la ndoa.
Kutokwa na harufu mbaya ukeni kwa kiasi kikubwa husababishwa na fangasi wa candida, japo sio kila mara ndio maana kuna umuhimu wa kutafuta chanzo cha tatizo la kunuka uke.
Kutoa harufu mbaya ukeni huweza kuambatana na dalili zingine kama vile; Miwasho sehemu za siri, hisia za kuungua sehemu za siri, michomo na kutokwa uchafu sehemu za siri.
Sababu Za Uke Kutoa Harufu Mbaya:
Zipo sababu nyingi zinazopelekea mwanamke kutokwa na harufu mbaya ukeni, baadhi ya sababu hizo ni pamoja na;
A) Magonjwa Ya Zinaa (Sexually Transmitted Diseases).
Mfano wa magonjwa ya zinaa ni pamoja na kisonono, kaswende, Trichomoniasis n.k. Magonjwa haya yasipotibiwa kwa wakati hupelekea mwanamke kutoa harufu mbaya ukeni.
B) Matumizi Mabaya Ya Dawa Za “Antibiotics”.
Hutumiaji kiholela wa dawa hizi bila ushauri au maelekezo ya wataaalamu wa afya (daktari) ni mojawapo ya sababu ya mwanamke kutoa harufu mbaya ukeni. Hivyo ni vyema mwanamke akafuata ushauri na maelekezo ya wataalamu wa afya kabla ya kutumia dawa za Antibiotics.
C) Kutozingatia Usafi Na Kutokwa Sana Na Jasho.
Ni wazi kwamba uchafu na kuwepo kwa unyevunyevu sehemu za siri huzalisha harufu mbaya.Kisayansi ni kwamba tezi zilizopo ndani ya mwili (Apocrine sweat glands) hutengeneza mafuta kuelekea kwenye maeneo ya mwili.
D) Maambukizi Katika Via Vya Uzazi (Pelvic Inflammatory Disease).
Pelvic Inflammatory Disease (PID) hili ni tatizo linalotokana na magonjwa sugu ya zinaa kama vile gonorrhea, chlamydia. Hivyo magonjwa ya zinaa ambayo hayakugundulika mapema, tiba hafifu, au uzembe wa kutumia dawa ni chanzo kimojawapo cha mwanamke kutoa harufu mbaya ukeni.
E) Bacterial Vaginosis.
Kwa kawaida mwili wa binadamu una bakteria wa aina mbili, bakteria rafiki (normal flora) na bakteria adui (pathogens) ambapo ukeni kuna bakteria rafiki kwa kiwango kinachohitajika, bakteria hawa wanapoongezeka na kuvuka mahitaji huwa sio rafiki tena, huanza kushambulia sehemu ya uke na kuruhusu maambukizi ambayo hutoa majimaji yenye harufu mbaya ukeni.
F) Mabadiliko Ya Homoni.
Mabadiliko ya homoni kutokana na mzunguko wa hedhi unaweza kuchangia harufu mbaya ukeni. Wanawake wanaokaribia kukoma hedhi (menopause) wapo kwenye hatari zaidi kwani homoni ya estrogen hupungua sana na hivo kusababisha tishu za kuwa na tindikali kidogo.