Fangasi ukeni kwa mjamzito ni mojawapo ya maambukizi kwenye uke yanawatokea sana wajawazito kutokana na aidha mabadiliko ya homoni za uzazi au mabadiliko ya mazingira ukeni (changes in vaginal pH).
Maambukizi ya fangasi ukeni kwa mjamzito hujulikana kwa kitaalamu kama vaginal candidiasis during pregnancy.
Kisababishi Cha Fangasi Ukeni Kwa Mjamzito:
Fangasi ukeni kwa mjamzito husababishwa na vimelea waitwao Candida albicans.
Fangasi aina ya candida wanapatikana katika maeneo mengi ya mwili ikiwemo ukeni, kwenye ngozi nk ambapo Katika hali ya kawaida ya mwili, fangasi hawa hawana madhara kabisa (normal flora) mpaka pale kinga ya mwili itakaposhuka au mazingira ya eneo husika kubadilika ndipo utaanza kuugua.
Wajawazito wanaugua sana fangasi kutokana na mabadiliko ya homoni za uzazi wakati wa mimba. Wakati wa ujauzito kinga ya mwili inaweza pia kushuka, homoni za uzazi (estrogen na progesterone) huongezeka zaidi ambapo vyote hivi vinachangia kwa fangasi ukeni kukua kupita kiasi na kuleta madhara.

Mambo Yanayoongeza Hatari Kwa Mjamzito Kupata Fangasi Ukeni:
Yafuatayo ni baadhi ya mambo yanayomuweka mjamzito katika hatari ya kupata fangasi ukeni;
1) Ongezeko Kubwa La Homoni Za Uzazi Wakati Wa Ujauzito.
Wakati wa ujauzito homoni za uzazi, estrogen na progesterone huongezeka zaidi hususani homoni ya estrogen ambayo husababisha ongezeko la glycogen na hii hufanya ongezeko la ukuaji wa fangasi hawa kwa kasi kubwa japo kuwa pia estrogen hupelekea ongezeko la wadudu walinzi,candida albicans.
2) Kushuka Kwa Kinga Ya Mwili Wakati Wa Ujauzito.
Ujauzito pia unaweza kushusha kinga ya mwili kwa mwanamke na hivyo kupelekea kuharibiwa kwa msawazo (changes in vaginal pH) kati ya ulinzi wa maeneo ya ukeni na fangasi aina ya candida albicans ambapo endapo wadudu walinzi (normal flora) aina ya lactobacilli wakipungua hupelekea ukuaji kupita kiasi wa fangasi na kupelekea dalili za ugonjwa wa fangasi.
3) Matumizi Yaliyokithiri Ya Dawa Za Kuua Bakteria (Antibiotics).
Endapo mama mjamzito anatabia ya kutumia dawa za kuua bakteria mfano dawa za kutibu ugonjwa wa UTI au dawa za kutibu magonjwa ya zinaa kiholela au kwa muda mrefu hupelekea kuharibiwa kwa msawazo (changes in vaginal pH) kati ya ulinzi wa maeneo ya ukeni na fangasi aina ya candida albicans ambapo endapo wadudu walinzi (normal flora) aina ya lactobacilli wakipungua hupelekea ukuaji mkubwa wa fangasi na hivyo kupelekea dalili za ugonjwa wa fangasi.
Madhara Ya Fangasi Ukeni Kwa Mjamzito:
Madhara yafuatayo yanaweza kutokea ikiwa mjamzito mwenye fangasi ukeni atashindwa kupata tiba mapema;
1. Mimba Kuharibika.
Hii hutokea kwa mama mjamzito ambaye hakupata tiba ya maambukizi ya fangasi ukeni mapema ambapo maambukizi hayo huenea sehemu mbalimbali za via vya uzazi na kuharibu mji wa mimba (uterus), sehemu ambapo mimba hujishikiza (fetal implantation) na kupelekea mimba kuharibika kabla ya wakati wake.
2. Kupata Homa Na Kizunguzungu.
Hali hii hutokea kwa sababu ya kubadilika kwa hali ya kawaida ya mwili na kuharibika kwa sehemu mbalimbali za mwili kutokana na maambukizi ya fangasi hali ambayo husababisha kubadilika kwa joto la mwili pia.
3. Kuongezeka Kwa Miwasho Sehemu Za Siri.
Madhara ya fangasi ukeni husababisha kuwepo kwa miwasho kwenye sehemu za Siri ambapo mwathirika hujikuna kila wakati, hali hii huongeza uwezekano mkubwa wa kuenea kwa ugonjwa wa fangasi ukeni kwa sababu mwenye maambukizi kama anajikuna na anawagusa wengine wanaomzunguka basi anaweza kusambaza maambukizi hayo kwa wanaomzunguka kwa urahisi.
4. Maumivu Makali Wakati Wa Kukojoa.
Hali hii hutokea kwa mgonjwa mwenye tatizo la fangasi ukeni, pale ambapo maambukizi yameenea sehemu mbalimbali za via vya uzazi na kusababisha michubuko. Hivyo wakati wa haja ndogo, mgonjwa akikojoa na mkojo ukagusa sehemu ya michubuko maumivu makali hutokea na kusababisha kukosa raha.
Jinsi Ya Kujikinga Na Fangasi Ukeni Kwa Mjamzito:
Yafuatayo ni mambo ya muhimu ambayo mjamzito anapaswa kuzingatia ili kujikinga na fangasi ukeni;
1. Vaa nguo za ndani ambazo hazibani na zilizotengenezwa kwa pamba au hariri.
2. Epuka kufanya mapenzi na mpenzi wako mwenye maambukizi haya mpaka pale atakapotibiwa na kupona kabisa.
3. Osha sehemu zako za siri kwa kutumia maji safi na jikaushe kwa kutumia taulo au kitambaa safi.
4. Epuka kuoga maji ya moto sana (hot baths), tumia maji ya vuguvugu.
5. Kula mlo wenye virutubisho kama vile mboga za majani, matunda.
6. Kunywa maziwa aina ya mtindi yenye live culture mara kwa mara yatakusaidia.
7. Epuka kutumia sabuni za kemikali au dawa kuoshea uke.
8. Usivae nguo zenye unyevunyevu, hakikisha unavaa nguo zilizokauka vizuri.
9. Epuka kutumia kiholela dawa za Antibiotics, kama huna ulazima wa kutumia antibiotics, acha kutumia.