TYLA awabwaga tena Wanigeria tuzo za BET

0:00

10 / 100

Mkali wa wimbo wa Water kutoka nchini Afrika Kusini
Tyla Laura Seethal maarufu kwa jina la Tyla, amenyakua tuzo yake ya kwanza ya BET katika hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia leo nchini Marekani.

Tyla amenyakua tuzo hiyo katika kipengele cha Best International Act na Best New Artist akiwapiku Tiakola, Asake, Cleo So, Focalistic, Karol Conká, Ayra Starr, Aya Nakamura BK’, pamoja na Raye.

Tlya aliwahi pia kushinda katika tuzo za Grammy 2023 kama Best African Music Performance kupitia wimbo wake wa Water akiwapiga chini Asake (Amapiano), Davido (Unavailable) ,Burna Boy (City Boys) na Ayra Starr (Rush).

Kwanini Wimbo wa Tyla ?

Kwenye tuzo kubwa za Mziki kama BET ni wazi ,wimbo wa msanii huwa unapata vigezo vya kuwa bora kwa kuzingatia sana asili ya mziki wake na sio umaarufu wala wingi wa wafuatiliaji (Followers) bali kuna vigezo vya kisayansi huzingatiwa. Wimbo wa Asake ni Amapiano ambao asili yake ni Afrika Kusini, wimbo wa Davido ni Amapiano pia,wimbo wa Ayra Starr ni Zuku kutoka Caribbean na Wimbo wa City Boys in Miracles wa Burna Boy ni Rap ambayo ni wazi kabisa ni mziki wa Marekani.

Wengi wamekuwa wakifikiri Tyla kashinda tu kwasababu ya wingi wa takwimu, la hasha! Lakini pamoja na yote hayo ni kweli wimbo wa “Water” una wingi wa Streams kwenye mtandao wa Spotify ukilinganisha na wasanii wenzake kwa zaidi ya Streams milioni 400 huku Streams za Davido na Burna Boy kwa ujumla hawajafika hata nusu yake.

Muundo wa Wimbo

  1. Wazalishaji wa wimbo wote ni washindi wa tuzo za Grammy kwa maana ya Waandishi,Waandisi wa sauti ( sound engineers). Wazalishaji wa wimbo huu ni Waingereza ambao pia uandika nyimbo za Beyonce na Rihanna ambao ni John Stewart na Lameck Sooth.
  2. Wimbo huu una gitaa la Acoustic guitar ambalo limepigwa na Mouzhukka
  3. Kinanda kikapigwa na Martial
  4. Maroon akapiga ngoma (drums)
  5. sauti ni Tyla,Jacob Redzma na Smith
See also  NYOTA WA MIELEKA VIRGIL JONES AFARIKI DUNIA

Wimbo huu kutoka Afrika Kusini umeingia kwenye chati za Billboard baada ya kupita miaka 55 tangu wimbo wa Masekele wa mwaka 1969.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

JINSI SERIKALI YA TANZANIA INAVYOTUMIA MABILIONI KWAAJILI...
MAKALA Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas...
Read more
IMPORTANCE OF SALES AND MARKETING IN BUSINESS.
Sales and marketing play a crucial role in the success...
Read more
Wojciech Szczęsny has announced his retirement from...
34-year-old ends his senior professional career which was 15 years...
Read more
Paris St Germain will not rush into...
Ramos injured his ankle in last weekend's 4-1 win at...
Read more
Aden Duale Expresses Gratitude for Defence Cabinet...
In a post on his X account, Nominated Defence Cabinet...
Read more

Leave a Reply