Kwanini Mahakama imemfutia Donald Trump mashitaka yanayomkabili?

0:00

12 / 100

WASHINGTON

Mahakama Kuu ya Marekani imeamua kwamba Donald Trump hawezi kushtakiwa kwa matendo ambayo yalikuwa ndani ya mamlaka yake ya kikatiba kama Rais katika uamuzi wa kihistoria unaotambua kwa mara ya kwanza aina yoyote ya kinga ya Rais dhidi ya mashtaka.

Majaji, katika uamuzi wa 6-3 ulioidhiishwa na Jaji Mkuu John Roberts, wametupilia mbali uamuzi wa mahakama ya chini ambao ulikuwa umekataa madai ya Trump ya kinga dhid ya mashtaka ya jinai ya shirikisho yanayohusiana na juhudi zake za kubatilisha kushindwa kwake na Rais Joe Biden katika uchaguzi wa 2020.

Majaji sita wasiopenda mabadiliko wameunga mkono uamuzi huo wa Mahakama Kuu, wakati watatu wa mrengo wa kushoto wamepinga.

“Tumehitimisha kwamba chini ya muundo wetu wa kikatiba wa kugawanya madaraka, asili ya mamlaka ya Rais inataka kwamba Rais wa zamani awe na kinga fulani dhidi ya mashtaka ya jinai kwa matendo rasmi wakati wa kipindi chake ofisini,” amesema Jaji Roberts.

Trump ni mgombea wa Chama cha Republican anayemkabili mgombea wa Democrat Rais Biden katika uchaguzi Mkuu wa Marekani Novemba 5, 2024 katika marudio ya uchaguzi wa 2020.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

BASIC QUALITIES MUST BE APPLIED IN MARRIAGE
LOVE TIPS ❤ MARRIED WOMEN AND MEN ONLY: Try your...
Read more
Milan's Morata house hunting again after mayor's...
AC Milan striker Alvaro Morata's plan to live in a...
Read more
Infectious Disease Expert Tapped as Kenya's New...
President William Ruto has nominated Deborah Mlongo Barasa as the...
Read more
10 TRAITS IN A WOMAN THAT ATTRACT...
❤ 1. GENTLENESSA woman who doesn't love drama, one who...
Read more
Nigerian man drags Ayra Starr for not...
CELEBRITIES
See also  MADAKTARI WAZAWA WATENGANISHA WATOTO MAPACHA WALIOUNGANA
Man takes to social media to call out Ayra...
Read more

Leave a Reply