UCHAMBUZI
Faida ya uwepo wa Chama Jangwani kwanza uzoefu wa mashindano ya kimataifa: kwenye kikosi cha Yanga hakuna mchezaji anafikia rekodi za Chama katika mashindano ya kimataifa kwenye ligi ya mabingwa barani Afrika
Amecheza misimu (6) michezo ( 55) Mabao 12
Anashika nafasi ya saba katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa ligi ya mabingwa barani Afrika na nafasi ya kwanza kwa wachezaji ambao bado wana emdelea kucheza mpira barani Afrika . hapo pia ana uzoefu wa kombe la shirikisho barani Afrika na Africa Football league (AFL) kumbuka ni mshindi wa kombe la shirikisho barani Afrika msimu 2021/22.
Chama akiwa Msimbazi ameipeleka Simba hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika zaidi ya mara mmoja kwa mabao kutoka mguni kwake ukiacha na ile ya linafungwa goli gani Simba dhidi ya Nkana mara ya kufanya hiyo mwisho ilikuwa msimu uliopita Simba dhidi ya power dynamos.
nikukumbushe jambo Yanga baada ya miaka zaidi ya 20 kupita msimu uliopita ndio walitinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika wakati huo Chama Akiwa Simba kwenye miaka 7 amefika hatua ya Robo faianali zaidi ya mara moja.Lakini huenda msimu ujao malengo ya Yanga ya kawa ni kufika hatua ya Robo fainali au nusu fainali kwasababu msimu uliopita walikuwa na malengo ya kufika makundi wakafika Robo fainali.
Watu wanasema hatopata nafasi ya kucheza inaweza ikawa kweli ila ntakupa mfano Jonas Mkude msimu uliopita hakucheza sana lakini mechi dhidi ya Mamelodi ilitosha kudhihirisha umuhimu wa uzoefu na huenda ilikuwa sababu tosha ya kuongezewa mkataba Jangwani . hivyo hata Chama hata asipopata nafasi sana bado anakitu chatofauti ambacho nyota wengine wanaweza wasiwenacho au anaweza kuwa msada kwa klabu pindi watakao kuwa wanapata nafasi kuosekana.
Umri miaka (33) Ni mkubwa inawezekana lakini katika umri huo bado anauwezo wa kuchangia mabao zaidi ya 20 akipewa dakika za kutosha kumbuka melengo ya timu ni kufanya vizuri hivyo una hitaji mtu atakae kusaidia kufanya vizuri kuliko kuangalia umri wake.
Siri imefichuka kwamba, kila kitu ambacho Chama alikuwa akiwasiliana na viongozi wa Simba wakimshawishi asaini mkataba alikuwa akimwambia Eng. Hersi.
Chama amesaini mkataba wa MIAKA (2) na Yanga SC baada ya mkataba wake kumalizika na Simba akigoma kuongeza mkataba na Simba SC sababu kubwa ikitajwa kuwa ni maslahi pamoja na kejeli za hapa na pale.”
“Yanga SC haikuwa imepanga kumtambulisha jana kama ambayo ilifanyika, lakini hatua hiyo ilitokana na matajiri hao (GSM & Hersi) kupokea simu kutoka kwa kiungo huyo kuwa Simba imepata uhakika kuwa yeye amesaini upande wa Yanga SC.”
“Kila kilichokuwa kinaendelea usiku wa jumapili baina ya Chama na viongozi wa Simba SC, Chama alikuwa anakishusha kwa Yanga kama kilivyo na ndiye aliyewashauri viongozi wa Yanga waachie picha yake asubuhi kabla ya chai kama kitendo cha kuwanyamazisha wasimsumbue.”
“… Chama anaamini hawakumuheshimu alipokuwa Simba”
“Ukweli mwingine ni kwamba Chama aliwaambia rafiki zake kuwa anataka kucheza ligi ya Mabingwa Afrika na Yanga inaonesha uelekeo wa kufika mbali”
“Simba SC baada ya kupata taarifa hizo matajiri wake kuanzia June 30 walirudi mezani wakihaha kumbakisha kiungo huyo kwa gharama yoyote wakimuwekea pesa mara mbili ya zile alizochukua Yanga, lakini ngoma ikadunda”
“Yanga baada ya kupata taarifa hizo (Kutoka kwa Chama) na kujiridhisha ikaona hapana isambaze picha hizo wakati akisaini kama walivyoshauriwa na Chama, zikawatibua mabosi wa Simba SC”
“Hata hivyo Simba hawakukata tanaa mpaka jana Jumatatu mchana waliendelea kusukuma kete ya mwisho kwa Chama wakimtaka akubali kusaini mkataba kisha wao wanajua namna gani watakwenda kumalizana na Yanga (TFF), lakini Chama akakataa”