Mzio hutokea pale mwili unapopambana na kitu kisicho na madhara kwa kawaida, kama vile poleni, manyoya ya wanyama, au vyakula fulani. Vitu hivi vinavyosababisha mzio huitwa “Allergens”.
Sababu zinazoweza kusababisha Mzio:-
🔴Urithi: Kama kuna historia ya mzio katika familia yako, kuna uwezekano mkubwa wa wewe pia kuwa na mzio.
🔴Mfumo wa Kinga mwilini kutofanya kazi vizuri: Mfumo wa kinga mwilini unapokuwa bado unakua unaweza kuathiriwa na vitu mtoto anapokutana navyo katika umri mdogo.
🔴Mazingira: Kukaa karibu na vitu vinavyosababisha mzio hewani kama vumbi kunaweza kusababisha mzio.
Muhimu: Ikiwa una dalili za mzio, ni muhimu kuonana na daktari kwa ajili ya uchunguzi na matibabu sahihi. Daktari anaweza kufanya vipimo kubaini ni nini kinachosababisha mzio wako na kupendekeza njia za kupunguza dalili, kama vile dawa.