SAMIA kubeba gharama za matibabu ya Sativa

0:00

10 / 100

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa atabeba gharama zote za matibabu ya kijana Edgar Mwakabela, maarufu kama Sativa kuanzia sasa mpaka atakapopona kabisa, pamoja na kuhakikisha unafanyika uchunguzi wa tukio la kutekwa kwake.

Hayo yameelezwa Kiongozi Mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto kabwe leo baada ya kumtembelea kijana Sativa ambaye aliyetekwa Jijini Dar es salaam June 23,2024 na kupatikana akiwa amejeruhiwa usiku wa kuamkia June 27,2024 katika Hifadhi ya Katavi ambapo amesema alifanya jitihada za kumtafuta Rais Dkt. Samia kuzungumza naye, kumuelezea tukio la Sativa kutekwa, kupigwa risasi na kutupwa msituni Katavi, pamoja na matukio mengine ya watu kupotea, ambayo yamekithiri katika siku za karibuni.

Zitto amesema kuwa amemueleza, yeye kama Rais na Amiri Jeshi Mkuu anao wajibu wa kulinda usalama wa Raia, na kwamba matukio ya namna hii yanachafua taswira na haiba yake, na yanaondoa murua wa R Nne zake (4R’s).

“Nimemsihi Ndugu Rais juu ya umuhimu wa yeye binafsi kuagiza ufanyike uchunguzi wa vyombo vya ulinzi na usalama juu ya tukio hili pamoja na mengine ya namna hii. Kama Taifa, tunahitaji kushirikiana pamoja kukomesha mambo ya watu kutekwa, kuuawa, kupigwa na kutupwa misituni, yeye Rais anapaswa kuwa wa kwanza kwenye hili.”

“Nduqu Rais amenisikiliza, na ameahidi kufanyia kazi ushauri wangu kwake. Na kama hatua ya awali amenieleza kuwa yeye binafsi atabeba gharama zote za matibabu ya Sativa, kuanzia sasa mpaka atakapopona kabisa, pamoja na kuhakikisha unafanyika uchunguzi wa jambo hili.”

“Ninamshukuru Ndugu Rais kwa mwanzo huu. Kila safari ndefu, inaanza na hatua ya kwanza. Naamini sasa tutaanza safari ya kwenda kule tunakotaka, ambako tabia za kutekana na kutesana zitakomeshwa. Mungu Ibariki Tanzania”

See also  TAARIFA ZA UONGO WALIZO NAZO WANAWAKE KUHUSU WANAUME.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Food vendor turned heads as he commemorating...
A 25-year-old man from Nigeria has caught the public's eye...
Read more
HESABU ZA SIMBA NA AZAM ZIKO SAWA
MICHEZO Bao pekee la mshambuliaji Fred Koublan limewawezesha wekundu wa...
Read more
"THERE'S SOMEBODY IN POWER THAT IS DATING...
LOVE ❤ Bobrisky power man dating verydarkmanPopular activist, Verydarkman debunks...
Read more
SABABU AL-HILAL OMDURMAN KUJIUNGA NA LIGI KUU...
MICHEZO Mkurungezi wa Bodi ya Ligi , Almas Kasongo amekiri...
Read more
AJALI ILIVYOUWA WATU 7 MOROGORO
HABARI KUU Watu saba wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa...
Read more

Leave a Reply