Leo sitaki maneno mengi, naingia moja kwa moja kwenye hizi taarifa nyeti nilizonazo.
Story inaanzia Chama akiwa amelala kitandani, nyumbani kwake Lusaka – Zambia. Mishale ya Saa 3:30 Usiku anapokea simu kutoka kwa tajiri, Mo.
Chama anapokea maelekezo ya tiketi ya ndege aliyokatiwa na Mo kuwa aende Dubai haraka sana kwa ajili ya maongezi ya kusaini Mkataba wa kusalia Simba.
Chama kwenye simu akamjibu Mo, kwanini nije Dubai wakati nimeshasajiliwa na Yanga na hela wameshanipa? Na nusu ya hela za usajili nmeshanunua kiwanja huku Zambia kwa ajili ya Mwanangu wa kiume.
Mo akamueleza Chama, wewe njoo Dubai haya yote yanazungumzika. Sasa kwa kuwa Chama ni mtu msikivu, mnyenyekevu, ana hofu ya MUNGU, mapema asubuhi akadandia pipa kwa tiketI aliyokatiwa na Mo akazama mjini Dubai.
Mo uso kwa uso na Chama.
Hiki kikao kilikua cha zaidi ya masaa manne, Mo akifanya juhudu za ushawishi Chama abaki Simba.
Taarifa nilizonazo ni kuwa hiki kikao lengo mahsusi lilikua;
1/ Chama asaini Simba mkataba wa miaka 2
2/ Chama alipwe pesa ya Usajili mara tatu zaidi ya ile aliyopewa na Yanga
3/ Chama apewe nyumba Masaki
4/ Chama alipiwe ada ya mwanae
Kikao hiki kilikua cha moto sana, Chama akishikilia msimamo kuwa ameshasajiliwa na Yanga, na itakua ngumu yeye kusaliti makubaliano.
Mo akamwambia Chama rudi zungumza na Hersi halafu tuone itakuaje?.
Jioni ya siku hiyo kwenye mida ya saa 1 kasoro saa za Dubai, Chama akampigia Injinia simu, akamueleza ofa aliyotoa Mo kuwa ni mara tatu ya Milioni 450 ambazo Yanga imempa Chama.
Yaani Mo yupo tayari kutoa Dola 550,000 1.3Billion ili Chama abaki Simba!
Hersi akamjibu Chama akamwambia, Mwambie Mo anipigie mimi nikuuze wewe kwao, maana pesa yangu umeshachukua na mkataba wa karatasi tano umesinya mwenyewe kwa dole gumba. Mpaka sasa wewe ni mchezaji wangu halali. Hivyo kama MO atakubali kununua huu mkataba, mimi nitakuachia uende.