Mwimbaji wa R&B na pop wa Marekani Usher Raymond IV (Usher ) ametoa hotuba ya kusisimua wakati akipokea tuzo ya mafanikio ya maisha katika Tuzo za BET zilizofanyika usiku wa Jumapili.
Katika hotuba hiyo iliyochukua karibu dakika 15, usher alielezea jinsi Baba yake alivyomtelekeza kwa kutompenda hata hivyo ameamua kumsamehe.
“Kufika hapa kwa hakika haikuwa rahisi, lakini imekuwa na thamani yake,” alisema Usher ambeye Oktoba mwaka huu atafikisha miaka 46.
“Tuzo hii ya mafanikio ya maisha, sijui, jamani, kama ni mapema sana kuipokea? Kwa sababu bado ninakimbia na kufyatua ngoma kama nilivyofanya nilipokuwa na umri wa miaka minane.”
Mwimbaji aliendelea kusema juu ya baba yake kuacha familia yake alipokuwa mtoto.
“Nilikuwa nikijaribu kuelewa jina hili ambalo mwanaume yule alinipa ambalo halikudumu kwa sababu hakunipenda,” alisema.
“Lazima uwe na moyo wa kusamehe ili kuelewa mitego na magumu ya kweli ya mtu mweusi huku Marekani na baba yangu, alikuwa zao hilo.”
Pia alitafakari maana ya sasa kuwa baba mwenyewe.
“Huu ni mwaka wa baba. Simama kwa ajili ya binti zako na wana wako na uongoze,” aliambia watazamaji katika ukumbi wa michezo wa Peacock huko Los Angeles, Marekani.
“Ni muhimu kuelewa kwamba baba ni muhimu sana.
“Kwa akina baba wote usiku wa leo nyumbani au kwenye hadhira ningependa ninyi nyote msimame kwa sekunde mbili tu kwa ajili yangu.
Wanaume kadhaa kwenye hadhira waliposimama, Usher alisema: “Hatuna nafasi ya kusema vya kutosha, ‘Baba nimefanya’, kwa hivyo hii ni ya wanaume wote huko nje kuwa majenerali wa wana wao. na motisha kwa viongozi wetu weusi wa baadaye – vijana.”