Clatous Chama aipa “Thank you “Simba kikubwa

0:00

10 / 100

Ni takribani kilomita 0.6 ametumia Clatous Chama kutoka Makao Makuu ya Klabu ya Simba SC, Msimbazi kwenda ‘Twiga Street’ Jangwani na hatimaye ‘Magician’ huyo ameaga rasmi.

Chama anayeufanya mchezo wa soka kuonekana kama kula ice cream ya maziwa au kunywa asali huku ukiwa na smartphone ukitizama picha za Hamisa Mobeto au Hashikiki,
ametumia miaka sita kuifikisha Simba robo fainali mara nne akiwa Msimbazi.

Yanga walimtambulisha Chama siku tatu zilizopita, hata hivyo barua ya Chama imejibu sintohamu za kwanini alishindwa kutokea kwenye hafla za kula keki, na kushindwa kubadili utambulisho wake Instagram.

“Baada ya miaka sita ya furaha, majivuno na malengo, hatma zetu zilizounganishwa zinachukuwa mkondo mwingine, sina cha kuwalipa zaidi ya heshima kwa kila mmoja wenu kwa mapenzi na kuniunga mkono kwa miaka yote na hakuna atakayebadili historia tuliyotengeneza pamoja,” ameandika Chama kwenye Instagram yake.

Sasa fundi huyo wa soka atawatumikia Wananchi msimu ujao.

Itoshe kusema Wanasimba wanapaswa kukubaliana na ukweli kuwa kipenzi chao kimetoka mitaa ya Msimbazi eneo la Kariakoo.

Baada ya kimya kingi, hatimaye Mwamba wa Lusaka Clatous Chota Chama ametoa ‘thank you’ kwa familia ya Simba Sc kupitia waraka wake kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii.

“Wapendwa familia ya Simba, Miaka sita iliyopita, nilikuja kwenu kama mgeni. Mlinipa kusudi na changamoto ya kuwa toleo bora zaidi ya nilivyokuwa.” ameandika Chama.

“Tuliteka ardhi hii pamoja, tukapanua eneo letu hadi sehemu nyingine za Afrika, na kilichobaki ni historia.”

“Baada ya miaka sita ya furaha, majivuno na kusudi, hatima zetu zilizounganishwa huchukua uelekeo tofauti. Sina chochote ila heshima kwa kila mmoja wenu kwa upendo na msaada mlionipa miaka yote hii, na HAKUNA MTU anayeweza kubadilisha historia tuliyotengeneza pamoja.”

“Wanasema shoo haijaisha mpaka mwanadada huyo mnene aimbe, na ninaamini huu wimbo unafaa muda kwenu. Nawatakia kila la kheri, na tutaendelea kuonana. Nguvu Moja.”

Aidha Chama amebadili wasifu (profile) kwenye mitandao ya kijamii kutoka kuwa mchezaji wa Simba Sc na kuwa mchezaji wa Yanga Sc.

See also  COMMON MONEY MISTAKES TO AVOID
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

KWANINI PAUL KAGAME ANAMHOFIA DIANE RWIGARA?
SIASA Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara ameondolewa kinyang’anyiro cha...
Read more
MKE WA RAIS WA MAREKANI AFARIKI DUNIA...
HABARI KUU. Mke wa Rais wa zamani wa Marekani Jimmy...
Read more
CASTER SEMENYA KURUDI MASHINDANONI AKIVUKA KIZUIZI HIKI
MICHEZO Mawakili wa bingwa wa Olimpiki mara mbili, Caster Semenya...
Read more
WANAWAKE WAPEWA USHAURI KWENYE SIKU YAO
HABARI KUU Kuelekea siku ya Wanawake duniani itakayofanyika March 8,...
Read more
yangq
leo
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply