Kwanini aliyechoma picha ya Rais Samia amefungwa miaka 2?

0:00

12 / 100

Mahakama ya wilaya ya Rungwe leo julai 4. 2024 imemtia hatiani Bw. Shedrack Yusuph Chaula mwenye umri wa miaka 24 kutumikia kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya shilingi millioni 5 kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni wa mujibu wa kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mtandaoni 2015.

Akisoma hati ya mashtaka mwendesha mashtaka wa serikali Rosemary Mgeniji mbele ya hakimu mkazi mkuu wa mahakama ya wilaya ya Rungwe Mh. Ramla Shehagiro ameeleza kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo 22/6/2024 katika kijiji cha Ntokela wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Imeelezwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka kuwa mshtakiwa huyo akiwa dukani kwake maeneo ya Ntokela alirekodi ujumbe wa video wenye maneno “Kwakuwa umeshindwa kutetea taifa lako lisiathirike na ushoga hii video inakuhusu wewe na si mtu mwingine” huku akijua kuwa taarifa hizo ni za uongo zenye kupotosha jamii.

Alipopewa nafasi ya kujitetea mahakamani hapo mtuhumiwa huyo Bw. Shadrack Chaula mkazi wa Ntokela amesema yupo tayari kutumikia adhabu yoyote atakayopewa na mahakama hiyo.

Upande wa jamhuri ukiongozwa na mawakili wa serikali Veronica Mtafya na Rosemary Mgeniji umeiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine kwani kitendo hicho kimetafsiriwa kama udhalilishaji kwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akitoa hukumu hakimu mkazi mkuu wa mahakama ya wilaya ya Rungwe Ramla Shehagiro amesema kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015 kifungu cha 16 amemtia hatiani kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka miwili au kulipa faini ya shilingi milioni tano. Hata hivyo mtuhumiwa amepelekwa gerezani kwenda kutumikia kifungo baada ya kushindwa kulipa faini.

See also  AHUKUMIWA MAISHA JELA KWA KUMLAWITI MTOTO WA MIAKA 4

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Breaking: Imo LP senator defects to APC
Ezenwa Onyewuchi, the Senator representing Imo East and a member...
Read more
SVEN BOTMAN APATA MAJERAHA YA GOTI
MICHEZO Beki wa Newcastle United, Sven Botman anatarajia kukaa nje...
Read more
Fire reportedly razes Dangote refinery
A section of Dangote Refinery is currently engulfed by fire. Explosions...
Read more
SAMIA AGUSWA NA MSIBA WA RAS KILIMANJARO...
HABARI KUU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe....
Read more
ALIYEMUUA MTOTO KISA KUMRUSHIA JIWE AKIOGA KUNYONGWA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply