Mambo 10 kisheria unapaswa kuzingatia kabla hujanunua gari kwa mtu. Fuatilia mwanzo mwisho uzi huu itakusaidia.
1.Hakikisha muuzaji anamiliki gari kihalali na ana haki ya kuliuza. Uliza kuona jina la gari na uhakikishe kuwa jina la muuzaji linalingana na jina lililo kwenye kwa blue card original. Kumbuka tuu mtu hawezi kuuza Mali isiyo yake kisheria.
2.Hakikisha majina yaliyopo kwa kitambulisho chake cha nida yanafanana na yaliyoko kwa blue card pamoja na Tin namba yake,unakikishe anakupa copy ya kitambulisho na uwe umeona original yake. Hii inakupa uhakika kuwa muuzaji wa hiyo gari ndio mmiliki hivyo kagua nyaraka kwa umakin
3.Hakikisha mnaandikishana kwa mkataba wa mauziano wenye taarifa zote za gari kama zinavyo someka kwa blue car ya gari. Usikubaliane naye kwa mdomo, hakikisha anakupa copy za passport zake mbili pamoja na copy ya kitambulisho. Ili uweze kubadili umiliki TRA.
4.Hakikisha gari haina madeni mbalimbali kama ya parking,madeni ya faini za barabarani, hakina kesi mahakamani ya traffic,Unatakiwa ku fanya search kupitia mfumo wa TRA itakusaidia sana kununua chombo ambacho hakina shida hivyo unapaswa kuwa na wataalamu wanaoyajua magari vizuri.
5.Fuatilia historia ya umiliki wa gari husika mwambie akupe nyaraka alizo nunulia ili asije akatumia hizo kuomba loss report akutapeli mali ulionunua na hakikisha habaki na nyaraka yeyote kuhusu hilo gari,Pia baada ya kuuziana tuu kimbia kubadili umiliki wa hilo gari ili iwe yako.
6.Hakikisha unajiridhisha na fundi wako juu ya usalama wa gari husika, mifumo yake, uimara wake, ubora wake, na madhaifu yake, maana muuzaji hawezi kukuambia kila kitu kuhusu chombo anachouza hii, ukigundua changamoto una nafasi ya kuacha au kuzungumza na mnunuzi kuhusu bei.
7.Hakikisha kama mnunuzi tengeneza mkataba unaokulinda kwa maana kisheria unakufanya kuwa salama, unatetea haki zako kama mnunuzi ndio maana unatakiwa kuandaliwa na mwanasheria mbobevu wa hizi mambo atakayeweka vipengele muhimu vya kukulinda mnunuzi
- Unatakiwa ujue gharama za usajili wa Gari mfano kubadili blue card (Motor Vehicle transfer fees)50,000 kupata kadi mpya (Fee for Duplicate Card) 50,000 na stamp duty tax ni 1% ya bei mliouziana hii ni lazima ulipie. Ndio umiliki uje kwako.
- Kama umependa elimu hii, like, retweet na share na wengine ili tukuletee elimu zaidi. Kama huja tu follow bhasi fanya kutu follow. Hakikisha pia unafuatilia kila siku kwa elimu na maada mbalimbali za kisheria.