Kwanini CAF Imemtoza Samuel Eto’o faini badala ya Kumfugia?

0:00

9 / 100

Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limemtoza faini ya Dola za Marekani 200,000 Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (FECAFOOT), Samuel Eto’o, kwa ukiukaji wa maadili, lakini likakosa ushahidi wa kutosha kuendelea na mashtaka yanayohusiana na madai ya upangaji wa matokeo.

CAF lilianzisha uchunguzi kuhusu mwenendo wa Eto’o mwezi Agosti mwaka jana baada ya kupokea “taarifa zilizoandikwa na wadau kadhaa wa soka wa Cameroon”.

Jopo la nidhamu la CAF liligundua katika uchunguzi wake kwamba Mwanasoka Bora huyo wa Afrika mara nne “amekiuka kwa kiasi kikubwa kanuni za maadili, uadilifu na uanamichezo” za CAF kwa kutia saini mkataba wa kuwa balozi wa kampuni ya kamari ya 1XBET.

Mawakili wa Eto’o wamesema watakata rufaa kupinga hukumu hiyo.

1XBET inadhamini vitengo viwili vya juu vya kandanda ya kulipwa ya wanaume nchini Cameroon na upande wa kimataifa wa wanaume na wanawake, huku kanuni za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), zikisema kuwa watu walio chini ya kanuni zake hawaruhusiwi kujihusisha na kamari.

Julai mwaka jana, kundi linalowakilisha vilabu vya wachezaji wasiocheza soka nchini Cameroon lilimtaka Eto’o kujiuzulu, likieleza wasiwasi wao juu ya uhusiano wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 43 na 1XBET na kuendelea kuongoza Shirikisho la Soka la Cameroon.

Wakati Eto’o amepatikana na hatia ya kukiuka sheria za CAF kimaadili, ameepuka adhabu inayohusiana na upangaji wa matokeo, huku jopo la nidhamu likisema hakuna uthibitisho wa kutosha.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona, ​​Inter Milan na Chelsea alikuwa anachunguzwa pamoja na Valentine Nkwain, Rais wa klabu mpya iliyopandishwa daraja ya Victoria United, kufuatia mazungumzo ya simu ya wawili hao yaliyokuwa yakijadili kurejea kwa Victoria kwenye Ligi Kuu kabla ya kuhakikishiwa kupanda daraja.

See also  NINI CHANZO CHA UHABA WA DOLA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI ?

Wote wawili hapo awali walikanusha kuhusika katika njama zozote za kuchakachua matokeo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

ORODHA YA MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI NA...
Na MUJUNI HENRYUhariri Hadi kufikia Augusti 16, 2024.Kanisa Katoliki lina...
Read more
PSG beat Strasbourg 4-2 to claim top...
Goals from Senny Mayulu, Marco Asensio, Bradley Barcola and Lee...
Read more
Activist Withdraws Lawsuit against Deputy President Gachagua...
The High Court has withdrawn a matter in which activist...
Read more
Kwanini Barcelona Imeshindwa Kumsajili Dani Olmo Mbele...
Habari za usajili zinasema Manchester City imetuma ofa kumsajili...
Read more
KANYE WEST AREJEA MJINI INSTAGRAM ...
NYOTA WETU. Rapa na mwanamitindo maarufu Kanye West ambaye alibadilisha...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply