Kamati ya uchaguzi ya Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) imeengua jina la Wakili Boniface Mwabukusi katika kinyang’anyiro cha kugombea kiti cha urais wa chama hicho.
Katibu wa kamati ya rufaa ya uchaguzi ya chama hicho Nelson Frank amesema baada ya kamati ya uchaguzi mnamo 24 June 2024 kutoa taarifa kwa wananchama kuhusiana na wanachama ambao walionekana wamekidhi vigezo vya kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho wapo wanachama ambao hawakuridhishwa na maamuzi ya kamati ya uchaguzi.
Nelson amesema wanachama hao waliamua kukata rufaa kwenye kamati yay a rufaa ya uchaguzi ya chama hicho ambapo kamati hiyo mnamo 06 July 2024 ilitoa maamuzi juu ya rufaa hizo ambapo jina la Boniface Mwabukusi limekuwa mongoni mwa majina yaliyoenguliwa bila kuweka wazi sababu zilizosababisha aenguliwe.
Awali Wakili Mwabukusi alikuwa ni miongoni mwa wagombea sita waliokuwa wakiwania kiti cha urais wa TLS na sasa baada ya kuenguliwa jina lake wamesalia wagombea watano.
Siku moja kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), kamati ua rufaa za uchaguzi ya chama hicho imemuengua wakili Boniface Mwabukusi kugombea urais, ikisema ana doa la kimaadili kinyume na kanuni za uchaguzi huo.
Katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Agosti Mwaka huu, Mwabukusi alikuwa miongoni mwa wagombea sita waliopitishwa na kamati ya uchaguzi ya TLS kugombea nafasi hiyo.
Wengine ni pamoja na Ibrahim Bendera (Ilala), Emmanuel Muga (Ilala), Revocatus Kuuli (Mzizima), Paul kaunda (Kanda ya Magharibi), na Sweetbert Nkuba (Kinondoni).
Mwabukusi aliyejipatia sifa kwa kupinga mkataba wa uwekezaji na uendelezaji wa bandari kati ya serikali ya Dubai na ya Tanzania, alifikishwa kwenye kamati ya Maadili ya Mawakili na Mwanasheria Mkuu wa Serikali akimlalamikia kwa kukiuka maadili ya uwakili.
Baada ya shauri lake kusikilizwa alikutwa na hatia na kupewa ongo Mei Mwaka huu.
Akizungumzia suala hilo Mwabukusi amesema rufaa yake ilisikilizwa kwa njia ya mtandao na kuambiwa na kamati hiyo kuwa amepoteza sifa ya kugombea.