9 / 100

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool na timu ya Taifa ya Brazil, Roberto Firmino amekuwa Mchungaji wa kanisa la Kiinjilisti ambalo alianzisha huko Meceio, Brazil pamoja na mkewe, Larissa Pereira.

Katika taarifa kwenye mitandao ya kijamii, Filmino na Larissa walisema tangu walipookoka na kubatizwa mwaka 2020 walitamani pia na watu wengine wauone upendo wa Kristo juu yao.

“Tangu kukutana kwa mara ya kwanza na Kristo, tamaa iliwaka mioyoni mwetu, tunataka watu wahisi upendo huu uliotufikia, sasa tuna hamu na wajibu mwingine kuwa wachungaji kwa niaba ya MUNGU” walisema wawili hao.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.