Askari wa Jeshi la Akiba maarufu kama “mgambo” ambaye jina lake halikufahamika kanisani kunusuru Maisha yake kwani baada ya kushushiwa kipigo na wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga.
Tukio hilo limetokea leo Julai 10,2024, eneo la soko la Buhongwa jijini Mwanza, wakati kikosi kazi hicho cha mgambo kilipokuwa kikikamata matunda ya machinga wanaofanya Biashara katika eneo hilo.
Akisimulia mkasa huo, Machinga katika eneo , Abdallah Mohamed amesema kikosi kazi hicho kimewasili Buhongwa saa 3:00 asubuhi ya leo na kuanza kuchukua matikiti na mananasi ya mfanyabiashara eneo hilo ndipo kikazingirwa na machinga na kuanza kushushiwa kipigo.
Baada ya kukimbilia kanisa la Katoliki Kigango cha Buhongwa, umati ulizingira kanisa hilo na kushinikiza mgambo huyo atolewe nje ili waendelee kumshushia kipigo kwa kile walichodai kuchoshwa na tabia ya mgambo hao kuwanyang’anya na kuharibu bidhaa zao.