Rais wa Kenya, William Ruto amesema yuko tayari kukabiliana na wapiga kura mwaka 2027 na kuonya wanaojaribu kuvuruga utawala wake.
Akijibu wito wa kujiuzulu kwa mara ya kwanza, Ruto alieleza kuwa Kenya ni nchi ya kidemokrasia ambapo viongozi huchaguliwa au kufutwa kupitia kura.
“Tujue ya kwamba ikifika 2027 tutakuwa na mtihani na hawa wananchi na kila mtu atakuja na kazi yake amefanya,” alisema.
Rais Ruto amewakumbusha wanaopinga uongozi wake kuwa wananchi ndio watoa maamuzi na hakuna haja ya mikwaruzano ya kisiasa ya sasa.
Alisema wanaomtaka ajiuzulu wanapaswa kushikilia farasi wao hadi 2027 ili kuamua hatima yake juu ya nguvu ya utendakazi wake.
“Hakuna haja ya kusumbuana sasa hivi tusubiri huo mtihani kila mtu afanye ili tuone walioshinda na waliofeli najipanga kwa hilo tukutane huko mbona hakuna shida.”
Rais alitoa wito kwa Wakenya kudumisha amani na kuepuka kusababisha ghasia zinazoweza kuvunja umoja wa taifa.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.