-Leo itafanyika draw ya mashindano ya CAF (Champion League na Confederation Cup) jumla ya timu 111 zitashiriki mashindano hayo ikiwa timu 59 zitashiriki klabu bingwa Afrika (CAF Champion League) na timu 52 zitashiriki kombe la shirikisho (CAF Confederation Cup).
-Tanzania Bara itawakilishwa na timu nne (4) Yanga na Azam zitashiriki klabu bingwa Afrika na Simba na Coastal zitashiriki kombe la shirikisho, Yanga, Azam na Coastal zitaanzia raundi ya awali (Preliminary) huku Simba itaanzia raundi ya kwanza na washindi wa jumla wa raundi ya awali watafuzu raundi ya kwanza na washindi wa jumla wa raundi ya kwanza wanafuzu makundi.
CAF CHAMPION LEAGUE
-Timu 59 ndio zitashiriki CAF Champion League na timu 5 (Alhy, Esperance, Mamelodi, Petro Luanda na TP Mazembe) zitaanzia raundi ya kwanza (59-5=54) timu 54 zilizobaki zitaanzia raundi ya awali (Preliminary). Kwenye timu 54 timu 4 (Yanga, Pyramid, CR Belozdad na Raja) zina pointi nyingi kwenye Club Ranking, timu 14 zina pointi chache kwenye Club Ranking na timu 36 hazina pointi kabsa kwenye Club Ranking. Hesabu iko hivi (54÷2 = 27) timu 27 ambazo zitashinda michezo ya jumla ya raundi ya awali zitafuzu raundi ya kwanza na zitaungana na timu 5 zinazoanzia raundi ya kwanza (27+5=32) zitacheza raundi ya kwanza.
-Kwenye Draw ya CAF Champion league kutakuwa na Pot 5 zenye timu 50 ambazo ni timu 36 ambazo hazina pointi kwenye Club Ranking na timu 14 ambazo zina pointi chache kwenye Club Ranking (36+14=50) timu hizo zitaungana na timu 4 (Yanga, Pyramid, CR Belozdad na Raja) ambazo zina pointi nyingi kwenye Club Ranking (50+4=54) kuanzia raundi ya awali zenyewe zazitakuwa kwenye Pot Bali zilishapangwa kabsa majina kwenye mechi husika kulingana na ukanda inakotoka.
-Yanga itapangwa na timu ambayo itatoka Pot 2 yenye timu 11 za (Vitalo ya Burundi , Solar7 ya Djibouti, Commercial Bank ya Ethiopia, Gor Mahia ya Kenya, APR ya Rwanda, El Merreick na Juba za Sudan, Dakadaha ya Somalia, Azam ya Tanzania, As Villa ya Uganda na JKU ya Zanzibar) kutoka ukanda wa CECAFA katika ukanda huu kutakuwa michezo 6 raundi ya awali kwa timu 11 zilizopo Pot 2 + Yanga washindi 6 wa jumla wa michezo ya awali watafuzu raundi ya kwanza.
-Azam FC itakutana na timu za ukanda wa CECAFA, (Yanga, Vitalo, Solar7, Commercial Bank, Gor Mahia, APR, El Merreick, Juba, Dakadaha, As Villa na JKU ) Iwapo Azam na Yanga hazitakutana raundi ya awali (Preliminary) zinaweza pia kukutana raundi ya kwanza (First) iwapo zote zitafuzu raundi ya kwanza na Azam ikiwa imepangwa katika mchezo namba 3 (Pot 1 vs Pot 1) kwani washindi wa michezo 6 ya ukanda wa CECAFA watacheza wao kwa wao yaani mchezo namba 3 vs 4 (Yanga walipo), mchezo 5 vs 6 huku mshindi wa mchezo namba 1 vs Al Ahly, na mshindi wa mchezo namba 2 vs Esperance.
CAF CONFEDERATION CUP
-Timu 52 ndio zitashiriki kombe la shirikisho (CAf Confederation Cup) timu 12 ambazo ni (RS Berkane, Simba, Stade Melien, Enyimba, Zamalek, El Masry, Sfaxien, As Vita, Asec, USM Alger, Sekhukhune na FC Lupopo) zitaanzia raundi ya kwanza huku timu 40 zitaanzia raundi ya awali (Preliminary) ili washindi 20 wa jumla wa michezo ya raundi ya awali waungane na timu 12 ambazo zitaanzia raundi ya kwanza (20+12=32) na kuwa timu 32 ambazo zitacheza raundi ya kwanza na washindi 16 wa jumla ya michezo ya raundi ya kwanza watafuzu makundi ya kombe la shirikisho.
-Kwenye draw kutakuwa na Pot 3 zenye timu 37 ambazo hazina pointi kwenye Club Ranking na timu 3 (Jaraaf, Otoho na Zesco) ambazo zina pointi chache kwenye Club Ranking zenyewe zimepangwa kabsa moja kwa moja kulingana na ukanda husika.
-Klabu ya Simba itakutana na washindi wa jumla wa michezo ya Pot 2 yenye timu za (CS Constantine ya Algeria, Rukinzo ya Burundi, Coffee ya Ethiopia, Police ya Kenya, Police ya Rwanda, Uhamiaji ya Zanzibar, Horseed ya Somalia, Jamus ya Sudan, Stade Tunis ya Tunisia, Kitara ya Uganda au Timu za Libya (1 & 2) baada ya michezo ya raundi ya awali ya Pot 2 washindi 6 wa jumla watafuzu kucheza raundi ya kwanza timu moja kati ya hizo 6 ndio itacheza na Simba.
-Coastal ambayo itaanzia raundi ya awali (Preliminary) imepangwa Pot 3 na timu za Bravo ya Angola, Orapa United ya Botswana, CD Lunda ya Angola, Black Bulls ya Msumbiji, Dyamos ya Zambia, Stellenbosch ya Afrika Kusini, 15 De Augosto ya Equatorial, Alice Port COM, Hotspurs Uswatini, Elgeco Plus ya Madagascar, na Forester SEY washindi 6 kutoka Pot3 watafuzu raundi ya kwanza.