Muigizaji mkongwe wa Marekani George Clooney ametoa wito kwa Rais Joe Biden kujitoa kwenye mbio za kuwania awamu ya pili ya Urais.
Clooney ambaye ni mfuasi wa Chama cha Democrats amesema kuwa hatua hiyo itawapa nafasi ya kumshinda Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump ambaye pia anagombea kiti hicho.
“Hatuendi kushinda na Rais huyu” amesema Clooney kwenye makala yake iliyochapishwa katika Gazeti la The New York Times.
“Nampenda Joe, kama Seneta, kama Makamu wa Rais na kama Rais, ninamuamini, ameshinda vita nyingi, lakini vita moja ambayo hawezi kuishinda ni vita ya kupigana na muda, wote hatuwezi kuishinda hiyo”.
Hivi karibuni Rais Biden amekuwa akikosolewa vikali baada ya kufanya vibaya sana kwenye mdahalo ambao matokeo yake yanaashiria kufeli kwake.
“Biden niliyemuona wiki 3 zilizopita sio yule wa 2010 wala sio wa 2020, amechoka, ndio yule ambaye wote mmemshuhudia kwenye Mdahalo” alisema Clooney.