Kwa mara nyingine tena Rais wa Marekani Joe Biden (81) amekosea jina la Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na kumuita “Rais Putin”.
Tukio hilo limetokea jana wakati akimtambulisha Rais Zelensky aliyekuwa akijiandaa kutoa hotuba yake katika mkutano wa NATO huko Washington nchini Marekani.
Hata hivyo, Rais Biden alijirekebisha mwenyewe kwa haraka na kutaja jina sahihi.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pamoja na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani wamemtetea na kusema kuwa ulimi wake uliteleza.
Aidha, mmoja wa maafisa wa kampeni za Biden ambaye hakutaka jina lake litajwe amenukuliwa akisema “uwezekano wa kushinda uchaguzi ni sifuri, angejitoa tu kwenye hizi mbio”.
Pia Rais Biden mapema alichanganya tena kwa kumuita mpinzani wake katika mbio za Urais Donald Trump kama Makamu wake wa Rais badala ya Kamala Harris.