Yanga wameununua mkataba wa mkopo wa Jean Baleke na Al-Ittihad 🇱🇾
Lengo la kwanza ya Yanga hata kabla ya kumsajili Joseph Guede katika dirisha dogo Januari 2023 ilikuwa Jean Baleke (23).
Waarabu wakawawahi wakamchukua Mshambuliaji huyo raia wa DR Congo 🇨🇩
Guede kaachwa kwa sababu Yanga wamempata waliyemtaka kabla hata ya Joseph Guede kusajiliwa.
ℹ️ Baleke ambaye ni mchezaji wa TP Mazembe hadi 2025, alisajiliwa kwa mkopo wa mwaka (1) na klabu ya Al-Ittihad 🇱🇾 kwa dau la $ 100,000 (Tsh 265 million).
Yanga wamewalipa Al-Ittihad pesa ya mkataba wa miezi (6) uliokuwa umebaki kwa sababu mchezaji huyo ilishinikiza kuondoka ili ajiunge na klabu ya Yanga.
Baada ya kulipa pesa hiyo pia wakaongea na klabu ya TP Mazembe, Baleke akasajiliwa na klabu ya Yanga kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja hadi June 2025.
ℹ️ Klabu ya Yanga imepanga kumnunua Baleke moja kwa moja mara baada ya mkataba wake wa mkopo kumalizika.
Atalipwa zaidi ya Tsh 15 million kwa mwezi.
Baleke ni MWANANCHI 🔰
Atatangazwa rasmi kuanzia leo.
… ⚙️ 𝗧𝗢𝗙𝗔𝗨𝗧𝗜 𝗬𝗔 𝗕𝗔𝗟𝗘𝗞𝗘, 𝗚𝗨𝗘𝗗𝗘
Jean Baleke (23) 🇨🇩 na Joseph Guede (29) 🇨🇮 ni aina tofauti kabisa ya washambuliaji. Hawafanani kiuchezaji uwanjani.
◉ Jean Baleke ana kasi, yuko haraka
◉ Joseph Guede hana kasi.
◉ Baleke ni presser mzuri | Anaweza kufanya pressing kwa muda mrefu.
◉ Joseph Guede sio presser mzuri.
◉ Joseph Guede ni mtulivu zaidi.
◉ Utulivu wa Baleke haujafikia wa Guede.
◉ Katika uwiiano wa kufunga magoli ukilinganisha na idadi ya mechi, Jean Baleke yuko juu ya Joseph Guede.
ℹ️ Gamondi anataka timu yake icheze kwa kasi wanapovuka mstari wa katikati, aina ya Mshambuliaji kama Guede utamlaumu kwa sababu hana kasi hiyo wakati wa counter attack.
Mfumo wa Gamondi ndio umemtoa Guede kwenye kikosi cha Yanga SC.
Washambuliaji aina ya Guede wasio na kasi kubwa ufurahi zaidi kucheza ndani ya box kusubiri huduma kutoka kwa viungo washambuliaji hasa Mawinga.. Gamondi hachezi hivyo anataka mshambuliaji pia ahusike kwenye build-up.
Aina ya mawinga anaowataka ni kama DUKE ABUYA Modern Inverted wingers ambao hawakumbatii sana chaki pembeni, wana cut in.. Sio kama Okrah au Kisinda ambao muda mwingi wanacheza na chaki.. Wapo makocha wenye falsafa tofauti na Gamondi hutaka aina hiyo ya mawinga.
Kwa mantiki hiyo bila shaka yoyote DUKE ABUYA atakuwa ni pendekezo la Gamondi.
Jean Baleke ni Mshambuliaji ambaye anafit kwenye mfumo wa Gamondi kwa sababu ana kasi na anaweza kuwa sehemu ya ujenzi wa mashambulizi bila kuathiri uwepo wake katika goli la mpinzani kwa kuwa ana kasi.
ℹ️ Rejea kwa Washambuliaji wa kigeni waliosajiliwa na Yanga baada ya Mayele kuondoka.
◉ Hafiz Konkoni.
◉ Joseph Guede.