Wasichojua vijana wengi moja ya siri ya mafanikio ni mwenza uliyenae. Ukiona mwanaume ana maendeleo mazuri mambo yake yako safi yamenyooka kwa asilimia 95 nakuhakikishia kuna mwanamke wa maisha yake nyuma yake anayempa support inayosaidia uchumi wake kuwa endelevu, lazima ana mahusiano yenye malengo ya maisha
Ni ngumu sana kijana bachela kuwa na wazo la kununua kiwanja kujenga ila akioa lazima awaze mambo ya msingi ya maendeleo, mke huwa mshauri mkuu nyuma yake. Ukiona mkaka ameanza kubadilika na kufanya mambo ya msingi mchunguze unaweza kukuta ashaoa au tayari ana mke wa malengo
Hapa ndio maana mabinti wengi wenye tamaa huishia kuzalishwa na waume za watu na kuwa single mothers maana wanapenda wanaume wenye magari na maendeleo kumbe tayari wana familia ndio maana uchumi wao ni endelevu.
Mwanamke wa malengo sio mchunaji bali mchangiaji kwenye maendeleo ya mumewe ndio maana vijana wahongaji /mabachela wengi maisha yao huwa hayaendi, familia ina nguvu sana kujenga uchumi endelevu ila UASHERATI NI CHANZO CHA UMASKINI