Mgombea wa Urais na mwanamageuzi Nchini Iran, Masoud Pezeshkian ameshinda uchaguzi wa Rais katika duru ya pili dhidi ya Mhafidhina Saeed Jalili.
Matokeo yaliyotangazwa na Wizara ya Mambo ya Ndani yanaonesha kuwa Pezeshkian amepata zaidi ya kura milioni 16 na Jalili amepata kura zaidi ya milioni 13 kati ya kura milioni 30 zilizopigwa ambapo watu waliojitokeza kupiga kura walifikia asimilia 49.8 kwa mujibu wa Msemaji wa Mamlaka ya uchaguzi Mohsen Eslami.
Viongozi mbalimbali Duniani akiwemo Rais Vladmir Putin wa Urusi na uongozi wa Saudi Arabia wametuma salamu za pongezi kwa Mwanamageuzi huyo kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Iran.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, Masoud Pezeshkian amewashukuru Watu wa Iran kwa kumchagua mwenye uchaguzi huo uliofanyima baada ya kifo cha Rais wa Iran Ebrahim Raisi katika ajali ya helikopta.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.