0:00
Ili kutengeneza au kuimarisha urafiki katika ndoa, jaribu kufanya yafuatayo:
- Sikiliza, sikiliza, msikilize: Jitahidi sana kusikiliza bila kukengeushwa, bila kutengeneza orodha ndefu ya mambo akilini mwako wakati anapoongea na bila kushughulishwa na chochote. Kumbuka anachokushirikisha kuhusu kazi, malengo yake, n.k.
- Zungumza naye mambo ya siku hiyo, muunge mkono na tengeneza mazingira ya maelewano.
- Angalia vipengele anavyovipenda, visome na ujiandae kuvizungumzia.
- Daima sema “TAFADHALI” na “AHSANTE”, hata kama ndoa yenu ina muda mrefu.
- Kuleni pamoja angalau mara moja kwa siku.
- Uwe msamehevu: Usitazame sana kasoro zake na jifunze kukumbuka sifa zake nzuri. Kila mtu anazo sifa hizo… hivyo weka macho na akili yako kwenye sifa hizo chanya.
- Panga shughuli za pamoja, kama vile kusafiri pamoja, kutembea pamoja, kula pamoja, kwenda nje pamoja… chochote ambacho mtakifurahia mkiwa pamoja.
- Chekeni pamoja: Usiufanye uhusiano wako na mumeo kuwa mkavu sana usiokuwa na hata maskhara na mzaha. Wanandoa wanaoweza kucheka pamoja, hudumu pamoja.
- Wekeni muda wa kujongeleana: kuwa na maingiliano ya karibu, kukumbatiana, kupakatana na kupapasana, huondosha vizuizi, hasira na hali ya kukata tamaa. Mara nyingi mtu hupata afueni baada ya kumbatio kubwa, maridhawa.
- Zungumzeni mambo mazuri: Iwapo utazungumza na rafiki yako kwa namna unavyozungumza na mwenza wako wa ndoa, je atabaki kuwa rafiki yako? Kuwa mkweli na jibu lako.
- Zingatieni usafi kabla ya kulala, na mlale wakati mmoja. Msiendeshe maisha ya kutengana.
HITIMISHO
Ndoa bora ni ile iliyojengwa kwenye msingi wa URAFIKI imara kati ya wanandoa
Related Posts 📫
The political future of Adan Bare Duale hangs in the...
Sometimes when two people have been dating or married for...
Manchester United captain Bruno Fernandes has avoided a three-match suspension...
LACK OF LOVELove is the greatest aphrodisiac; when you are...
Two players had tested positive on Tuesday. Meares added that...
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.