Milio inayokisiwa kuwa risasi imesikika kwenye mkutano wa hadhara wa Donald Trump huko Pennsylvania wakati rais huyo wa zamani alipokuwa akitoa hotuba.
Alikimbizwa nje ya jukwaa haraka na maafisa wa kitengo cha Secret Service.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump alitolewa nje ya jukwaa baada ya milio ya risasi kuzuka katika mkutano wa hadhara huko Pennsylvania katika jaribio la kutaka kumuua.
Picha zilimuonyesha akiwa na hasira na kuinua mkono kwenye sikio lake la kulia, kabla ya kuinama -huku mfululizo wa milio ya risasi ikisikika.
Upesi alivamiwa na maajenti wa Huduma ya Secret Service wanaomlinda na kuvutwa kutoka jukwaani hadi kwenye gari linalomsubiri. Aliinua ngumi huku akiingizwa kwenye gari.
Katika chapisho kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump alisema risasi ilipenya “sehemu ya juu” ya sikio lake la kulia. Hapo awali, msemaji wake alisema “anaendelea vizuri” na anapokea matibabu katika kituo cha matibabu cha eneo hilo.
“Nilijua mara moja kuwa kuna kitu kibaya kwa kuwa nilisikia sauti ya mlio, milio ya risasi, na mara moja nikahisi risasi ikipasua kwenye ngozi,” Trump aliandika. “Nilivuja damu nyingi, kwa hivyo niligundua kile kinachotokea.”
Damu zilionekana wazi kwenye sikio na uso wa Trump huku maafisa wa ulinzi wakimkimbiza.
Mshukiwa huyo alipigwa risasi na kufa katika eneo la tukio na maafisa wa Secret Service, msemaji wa shirika hilo Anthony Guglielmi alisema. Aliongeza kuwa mtu mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi na wengine wawili kujeruhiwa vibaya.Idara ya upelelezi nchini Marekani (FBI) imetoa taarifa za mtuhumiwa wa jaribio la mauaji ya Rais wa Zamani Donald Trump ambaye ametambulika kwa jina la Thomas Matthew Crooks mwenye Umri wa miaka 20.
Baadhi ya video zimemuonesha mtuhumiwa huyo aliyekuwa juu ya jingo ambapo baadhi ya mashuhuda wamekiri walimuona.
Hali ya Trump inaendelea vizuri kwa sasa baada ya kushambuliwa wakati wa mkutano wake wa hadhara katika Jimbo la Pennysylvania Nchini Marekani.Rais wa Marekani Joe Biden amelaani jaribio la kumuua rais wa zamani wa taifa hilo Donald Trump, akitoa wito kwa Wamarekani wote kukemea matukio kama hayo.
Rais Biden ametoa wito huo muda mchache baada ya tukio hilo la mtu mwenye silaha kumpiga risasi sikioni Trump, kumuua mwanachama mmoja na kuwajeruhi wengine wawili katika mkutano wa hadhara huko Butler, Pennsylvania.
Mshambuliaji huyo aliuawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa Secret Service.
Katika taarifa iliyotolewa ndani ya saa moja baada ya shambulio hilo, Bw Biden alisema “hakuna nafasi Marekani kwa hili. Ni lazima tuungane kama taifa moja kulaani. Ni mgonjwa, ni mgonjwa”.
Shambulio hilo lilijiri huku kukiwa na ushindani mkali wa uchaguzi kati ya wawili hao.
Biden ametoa kauli hiyo kupitia televisheni kutoka nyumbani kwake huko Delaware na kuongeza kuwa “kila mtu lazima alaani” matukio ya vurugu huko Butler.
“Hatuwezi kuruhusu hili lifanyike. Hatuwezi kuwa hivi. Hatuwezi kuunga mkono hili,” aliongeza.
Alisema anashukuru kusikia kwamba yuko salama na anaendelea vizuri.
“Ninamuombea yeye na familia yake na wale wote walio kwenye mkutano huo, Mimi na Jill [Biden] tunashukuru Huduma ya Siri kwa kumfikisha salama” aliongeza.“Nilipigwa risasi na risasi iliyopenya sehemu ya juu ya sikio langu la kulia,” Bw. Trump alisema katika chapisho kwenye kwenye mtandao wa Truth Social (mtandao wake wa kijamii).
“Nilijua mara moja kwamba kulikuwa na tatizo kwa kuwa nilisikia sauti ya mlio, milio ya risasi, na mara moja nikahisi risasi ikipasua kwenye ngozi” ameongeza Trump
Trump ametoa kauli hiyo baada ya shambulio la risasi dhidi yake alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za kuwania Urais wa taifa la Marekani huko Pennsylvania mnamo 13 July 2024.
Alikimbizwa nje ya jukwaa haraka na maafisa wa kitengo cha Secret Service.
Picha zilimuonyesha akiwa na hasira na kuinua mkono kwenye sikio lake la kulia, kabla ya kuinama -huku mfululizo wa milio ya risasi ikisikika.
Katika tukio hilo mtu mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi na wengine wawili kujeruhiwa vibaya.