“𝗬𝗮𝗻𝗴𝗮 𝗶𝗻𝗮𝘀𝗮𝗷𝗶𝗹𝗶 𝗸𝗶𝗺𝗮𝗵𝗲𝘀𝗮𝗯𝘂 𝘀𝗮𝗻𝗮 ..Kuna wakati nilikuwa najiuliza, hivi vilabu vyetu vikubwa hawamuoni Duke Abuya? Anajituma sana ,ana ufundi mkubwa, anacheza nafasi zote za mbele,zote za kati na ulinzi wa pembeni pande zote mbili, na kote huko anakupa katika ubora wa hali ya juu… Ukiutazama usajili wa Yanga unakwenda kujibu changamoto za msimu uliopita:”
“1- 𝗞𝘂𝘀𝘂𝗺𝗯𝘂𝗹𝗶𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝘁𝗶𝗺𝘂 𝘇𝗶𝗻𝗮𝘇𝗼𝗽𝗮𝗸𝗶 𝗯𝗮𝘀𝗶 ..Timu kama Kagera Sugar,JKT Tanzania na Tanzania Prisons ziliwapa Yanga wakati mgumu kuzifungua. Wachezaji kama Clatous Chama na Duke Abuya wana uwezo mkubwa wa kuifungua beki iliyo compact kama tu alivyo Paccome. Mechi za hivi wakati mwingine unahitaji watu wenye uwezo wa kupiga kutokea mbali,Prince Dube ana huo uwezo akiungana na Ki Aziz.”
“2 – 𝗠𝗲𝗰𝗵𝗶 𝘇𝗶𝗻𝗮𝘇𝗼𝗵𝗶𝘁𝗮𝗷𝗶 𝗸𝘂𝗴𝗼𝗻𝗴𝗮𝗻𝗮 𝗮𝘂 𝗺𝘁𝘂 𝗺𝗺𝗼𝗷𝗮 𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗸𝗮𝗮 𝗺𝗯𝗲𝗹𝗲 𝗽𝗲𝗸𝗲 𝘆𝗮𝗸𝗲 .. Jean Baleke ana uwezo mkubwa wa kusimama kama mshambuliaji pekee. Kuna wakati Kocha Gamondi anataka timu icheze 4-2-3-1, kwa usajili huu punda mbeba mzigo yupo.”
“3 – 𝗠𝗲𝗰𝗵𝗶 𝘇𝗶𝗻𝗮𝘇𝗼𝗵𝗶𝘁𝗮𝗷𝗶 𝗸𝗶𝗹𝗮 𝗺𝗺𝗼𝗷𝗮 𝗮𝗸𝗮𝗯𝗲 𝘀𝗮𝗻𝗮 𝗻𝗮 𝗸𝘂𝗸𝗶𝗺𝗯𝗶𝗮 𝘀𝗮𝗻𝗮.. Hizi ndio zile show za akina Kennedy Musonda, Mudathir Yahya na Maxi Nzengeli. Mfano mzuri ni mechi dhidi ya Mamelodi Sundown na Al Ahly. Chadrack Boka, Duke Abuya na Jean Baleke wanafaa sana kwenye mechi za aina hii”
“4 – 𝗦𝗶𝗸𝘂 𝘁𝗶𝗺𝘂 𝗶𝗻𝗮𝗵𝗶𝘁𝗮𝗷𝗶 𝘄𝗮𝘀𝗵𝗮𝗺𝗯𝘂𝗹𝗶𝗮𝗷𝗶 𝗮𝘀𝗶𝗹𝗶𝗮 𝘄𝗮𝘄𝗶𝗹𝗶 .. Kuna wakati Gamondi anapenda kutumia mfumo wa 3-5-2, hizi ndio zile siku za Clement Mzize na Joseph Guede walikuwa wanaanza pamoja,kombinesheni ilikuwa haijakolea sana. Prince Dube na Jean Baleke wanaweza kuifanya kazi hii vizuri sana kwa sababu Dube ana uwezo wa kuibia pembeni kidogo huku Baleke akisaidia kuimarisha muundo na uti wa mgongo wa timu kwa kutulia kati.”
“5 – 𝗞𝗶𝗯𝗶𝗮𝘀𝗵𝗮𝗿𝗮 𝗸𝘂𝗻𝗮 𝘀𝗼𝗸𝗼 𝗹𝗶𝗻𝗮𝗳𝘂𝗻𝗴𝘂𝗸𝗮 .. Asilimia 90% ya rafiki zangu wenye uraia wa Kenya ni mashabiki wa Yanga na ni wanunuaji wazuri sana wa jezi. Kutua kwa Abuya Yanga kutaongeza ufuatiliwaji wa Yanga nchini Kenya na kufungua zaidi mlango wa biashara kama ilivyo Congo na South Africa. Hii inaitwa Sir Alex Ferguson Approach.”
“Lakini wakumbusheni wageni wote wanaokwenda Yanga kuwa namba zote zina wenyewe, wanatakiwa wakapambanie.