0:00
Jumapilli 14/7/2024 dunia ilitaharuki kusikia huko Marekani, mgombea urais wa chama cha Republican, Donald Trump amepigwa risasi jukwaani wakati wa mkutano. Mrusha risasi aliuawa pale pale.
Wagombea wote yaani Rais wa sasa Joe Biden na Donald Trump wanaomba kuongoza kwa miaka mingine minne (Minne Tena). Trump ni kama alisahau kitu White House na Biden ni kama kuna kitu hajafanya, anatamani apate muda zaidi ili akifanye. Kijiwe cha Karagwe kinatafakari haya kuhusu mchuano huu:
- Risasi aliyopigwa Donald Trump ni “kura ya risasi” kuliko kuwa “risasi ya kura”. Wapo watakaompa kura kwa sababu ya kupigwa risasi. Tujiepushe na zimwi la risasi kwa wapinzani wetu. Risasi hugeuka kuwa kura.
- Kifungo na risasi ni viwanda vya kura katika chaguzi. Hata mgombea bomu akipigwa risasi wakati wa kampeini au kuwekwa mahabusu, kura zake huongezeka.
- Dhana hii ya namba 2 inawafanya baadhi ya watu waamini kuwa huenda Trump alipanga apigwe risasi ili kuongeza kura zake.
- Trump na Biden wote ni wazee. Biden anasahau njia ya kupanda ngazi kuingia kwenye ndege wakati Trump anasahau anagombea kuwa nani kwa sababu bado anajiona ni rais!
- Wagombea wote wawili wanadhihirisha kitu kimoja muhimu: Marekani inaongozwa na taasisi kuliko watu. Hata chizi anaweza kuwa rais wa Marekani kwa sababu si yeye anayeongoza.
- Uhuru usio na mipaka unastawisha utumwa wa taasisi; yaani taasisi inamtumikia mtu si mtu kutumikia taasisi. Uhuru kama wetu wenye mipaka unakuza utumwa mstaarabu (uchungu bila maumivu). Tunahitaji kuazimana lakini tukumbuke kurudisha.
- Risasi ni silaha ya mkandamizaji. Mkandamizwaji hutumia meno na ulimi. Anayekuuzia risasi leo, kesho anamuuzia adui yako fulana ya kuzuia risasi aliyokuuzia jana. Tunahitaji vita ya maneno siyo risasi. Hakuna fulana ya kuzuia maneno.
- Kutumia risasi kumnyamazisha Trump ni kumpendelea. Trump ni zao la “ndoto ya Amerika” inayoamini katika kutumia risasi kuzima ndoto nyingine. Ndoto ya Amerika inazimwa na ndoto ya Amerika (kufugia chatu kwenye chungu cha mfinyanzi).
- Trump si tatizo. Wanaomfuata ndio tatizo. Hakuna kazi nzito kama kumbadili muumini aliyemwamini nabii/mtume feki. Ataacha wali ale kinyesi na awacheke wanaomshangaa. Kampeini za Amerika hazina “unatuachaje” bali “Amerika kwanza” na Mungu baadaye.
- Kimsingi vyama vya Republican na Democrat vimekosa wagombea. Trump na Biden ni makuadi wa kuuza ndoto ya Amerika kwa nchi zisizo na ndoto zake. Gulio humnufaisha muuzaji kuliko mnunuzi. Wote wawili wanakubaliana kuwa na Amerika imara hata kama wao si imara kiakili na kimwili.
Ukimgeuza sana nyoka, utaona miguu yake.
Related Posts 📫
What Is Market Research?
The term market research refers to the...
According to a statement by NAF spokesman AVM Edward Gabkwet,...
According to Minister of Information and National Orientation, Mohammed Idris,...
MAGAZETI
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
NYOTA WETU
Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamnu Muhimbili...