Nini Kinaendelea Kuhusu Rais wa Yanga Hersi Said?

0

0:00

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam imetoa amri ya kuachia ngazi kwa Uongozi wa Club ya Yanga ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi na wenzake na kuondoka klabuni hapo kwakuwa Katiba ya Yanga haitambui uwepo wao.

Inaelezwa kuwa uamuzi huu wa Mahakama umekuja baada ya Kundi la Wazee wachache waliowahi kuwa Wazee wa klabu hiyo kipindi cha nyuma kupeleka mashitaka Mahakamani likidai uwepo wa Viongozi wa sasa wa Yanga Sc ni batili na haujafuata Katiba ya Club hiyo.

Kutokana na Wazee hao kushinda kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inamaana kuwa Rais wa Yanga Injinia Hersi na Viongozi wenzake wanatakiwa kuachia ngazi na kukabidhi Ofisi kuanzia sasa.

Injinia Hersi alianza kuiongoza Yanga kama Rais miaka miwili iliyopita baada ya kushinda nafasi hiyo akiwa ni Mgombea pekee July 2022 na kumfanya kuwa Rais wa kwanza wa Yanga SC toka kuanza kwa mfumo mpya wa mabadiliko ambapo alitangazwa kuwa atakuwa madarakani kwa miaka minne (hadi 2026 ) kwa mujibu wa Katiba ya Club hiyo.

Hata hivyo,𝗠kurugenzi wa Sheria wa Klabu hiyo,wakili Simoni Patrick ametoa ufafanuzi huu:-
.
“Tumegundua kuna kundi la watu linalowatumia hawa watu kuvuruga amani na tayari klabu kushirikiana na Vyombo vya Usalama tumeanza kuwafanyia uchunguzi hawa watu ambao wako nyuma yao.”

“Ikibainika wote watapelekwa mbele ya mkutano Mkuu kama ni wanawachama mkutano mkuu utachukua hatua,”

“Mnamo tarehe 6/11/2022 watu wawili waliojiita Wanachama wa Young Africans SC walifungua kesi Mahakama ya Kisutu, Bwana. Juma Ally pamoja na Geofrey Mwipopo. Walifungua kesi dhidi ya Wajumbe wa Baraza la Wadhamini ambao ni Mama yetu Fatma Karume, Abeid Mohamed Abeid na Mzee Jabir Katundu kwa madai ya kuwa hawalitambui baraza la wadhamini la Klabu ya Young Africans SC, wakidai liliingia kwa mujibu wa Katiba ya 2010(ambayo wanadai haijasajiliwa)”

See also  The embattled former Governor of the Central Bank of Nigeria, Godwin Emefiele, has initiated legal actions to contest the court-ordered forfeiture of his assets to the Federal Government.

“Mei 2024 walalamikaji walipeleka maombi ya kukazia hukumu kwa Hakimu Mkazi Kisutu, kuomba Mahakama kulifuta baraza la wadhamini wa Yanga na kuutoa uongozi wa Yanga na kutaka wakabidhiwe timu na Asset zote za Yanga waendeshe wao.”

“Baada ya kufanya hivyo Juni 10, 2024 klabu ilipata taarifa kwamba kuna kundi la watu wamepeleka maombi Mahakami kuomba uongozi wa Yanga uondolewe na wakabidhiwe klabu hiyo.”

“Uongozi wa Yanga chini ya Rais Eng. Hersi na Jopo la mawakili tulianza kufuatilia suala hilo na kugundua kuwa, kesi hiyo iliendeshwa kwa upande mmoja kwa hawa watu kugawana majukumu kwa upande wa mlalamikaji na mlalamikiwa.”

“Tuligundua Juma Ally Abeid aligushi sahihi ya Klabu na kujifanya mwenyekiti wa baraza la wadhamini wa klabu, aligushi sahihi ya Mama Fatma Karume akijidai mwakilishi wake, aligushi sahihi la Mzee wetu Jabil Katundu ambaye alilazimishwa kuingia kwenye hili shauri,”

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading