𝗠𝗔𝗔𝗗𝗛𝗜𝗠𝗜𝗢
Suala la Magoma limefungwa hivi :
ℹ️ Rais wa Yanga Eng. Hersi Said, kamati ya Utendaji ya Yanga na Bodi ya wadhamini wanaendelea na majukumu yao yote kama kawaida kwa sababu waliingia madarakani kupitia katiba halali iiyopewa baraka na Serikali pamoja na TFF ›› (FCC, BMT)
ℹ️ Young Afticans Sports Club imefungua kesi ya Jinai Kisutu dhidi ya Juma Magoma na wote waliohusika KUGHUSHI saini za wajumbe wa Bodi ya wadhamini, Mama Fatma Karume na mzee Jabil Katundu.
Pia Magoma na wenzie watapelekwa mbele ya mkutano Mkuu kama ni wanawachama halali mkutano mkuu utachukua hatua ya kuwafuta UANACHAMA kwa mujibu wa katiba ambayo inakataza masuala ya kikatiba na Migogoro yoyote ya kimpira ndani ya Yanga kupelekwa mahakamani.
ℹ️ Yanga SC imeiaandikia barua Mahakama isongeze mbele muda wa Klabu hiyo kufanya mapitio ya kesi kwa sababu haikuwahi kushiriki kwenye kesi hiyo.
𝗞𝗪𝗔 𝗡𝗜𝗡𝗜 𝗠𝗔𝗛𝗔𝗞𝗔𝗠𝗔 𝗜𝗟𝗜𝗧𝗢𝗔 𝗛𝗨𝗞𝗨𝗠𝗨 𝗕𝗜𝗟𝗔 𝗞𝗨𝗪𝗘𝗣𝗢 𝗞𝗪𝗔 𝗪𝗔𝗦𝗛𝗜𝗧𝗔𝗞𝗜𝗪𝗔 ?!
ℹ️ Kwa kuwa maombi ya mleta maombi (Juma Magoma) hayakupingwa, Mahakama ilikubaliana na nafuu zote zilizoombwa kwenye hati ya madai (PLAINT).
Maana yake washitakiwa Yanga SC hawakushiriki katika kesi hiyo tangu ilipofunguliwa Nov 2022 kabla ya Hersi Said na uongozi uliopo kuingia madarakani.
𝗠𝗦𝗜𝗡𝗚𝗜 𝗪𝗔 𝗞𝗘𝗦𝗜 :
ℹ️ 6/11/2022 Magoma na Geofrey Mwipopo walifungua kesi dhidi ya Wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa Yanga kwa madai kuwa hawalitambui baraza la wadhamini la Klabu hiyo wakidai liliingia kwa mujibu wa Katiba ya 2010 ambayo wanadai haijasajiliwa.
2 August 2023 Mahakama ya Kisutu ilitoa hukumu ikiwa imesikiliza upande mmoja.. hukumu hiyo haikutekelezwa na Yanga. Mei 2024 Magoma na wenzie walipeleka maombi ya kukazia hukumu kwa Hakimu Mkazi Kisutu, kuomba Mahakama kulifuta baraza la wadhamini wa Yanga na kuutoa uongozi wa Yanga na kutaka wakabidhiwe timu na Mali zote za Yanga waendeshe wao.
Wao wanaamini katiba ya mwaka 1968. Katiba iliyofanyiwa marekebisho 2011 na 2021 hawaitambui kwa hiyo mambo yote yaliyofanyika kuanzia 2010 hadi leo waliiambia mahakama iyabatilishe