Kwanini Yanga Inachelewa Kumtangaza Mshambuliaji Jean Baleke?

0

0:00

Wanaochelewesha mshambuliaji Jean Baleke (23) kutangazwa na Young Africans ni Jeunnesse Sportive de Kinshasha (JSK) 🇨🇩

ℹ️ DR Congo wana mifumo tofauti kidogo na Nchi nyingi kuhusu umiliki wa wachezaji.

Wachezaji wengi waliopo katika vilabu mbalimbali DR Congo wanamilikiwa na watu binafsi, Agency na Academy..

.. kwa hiyo ukiuziwa mchezaji au ukipewa kwa mkopo lazima pia umalizane na watu wanaommiliki mchezaji huyo.

ℹ️ Yanga walishamalizana na Al-Ittihad 🇱🇾 na TP Mazembe 🇨🇩 kuhusu Baleke.

JSK ambao ndio walimuuza Baleke TP Mazembe January 2021 kwa mkataba wa miaka mitano (5) wanataka pia pesa, ndio wanaochelewesha utambulisho wake.

Wakati anauzwa alikuwa na miaka (19).

Yanga wako hatua za mwisho kumalizana nao na huenda Baleke atatangazwa Yanga kabla dirisha la usajili la (CAF) halijafungwa.

ℹ️ Bado siku moja dirisha lifungwe.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  50 Cent bado aendelea kumkomalia Sean Combs "P Diddy "
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading